Sokwe (Hominidae)
Mandhari
Sokwe | ||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||
Jenasi 4:
|
Sokwe mkubwa au sokwe peke yake ni jina la binadamu na nyani wakubwa wa familia Hominidae wanaofanana sana na binadamu. Tofauti na nyani wengine ni kuwepo kwa mkia; karibu nyani wote huwa na mkia lakini masokwe wakubwa hawana kabisa. Binadamu (Homo) anahesabiwa pia kama jenasi yenye spishi moja katika familia hii.
Eneo na uenezaji
[hariri | hariri chanzo]Masokwe wasiokuwa wanadamu wanaishi katika maeneo ya tropiki ya Afrika (masokwe mtu na ngagi) na Asia (orangutanu). Wote ni wakazi wa misitu ila tu masokwe mtu wanaoingia pia kwenye mbuga au savana. Wanadamu wanaishi duniani kote kwa kubadili mazingira yao, kuvaa nguo na kujenga majumba yanayowalinda kutoka joto kali ama baridi.
- Ponginae (Ponginae)
- Orangutanu, Pongo
- Orangutanu wa Sumatra, Pongo abelii (Sumatran orangutan)
- Orangutanu wa Borneo, Pongo pygmaeus (Bornean orangutan)
- Orangutanu wa Tapanuli, Pongo tapanuliensis (Tapanuli orangutan)
- Orangutanu, Pongo
- Homininae (Homininae)
- Gorillini
- Ngagi, Gorilla
- Ngagi Mashariki au Gorila Mashariki, Gorilla beringei (Eastern gorilla)
- Ngagi-milima, Gorilla b. beringei (Mountain gorilla: Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda na Uganda)
- Ngagi wa Uwanda wa Chini Mashariki, Gorilla b. graueri (Eastern lowland gorilla: Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo)
- Ngagi Magharibi au Gorila Magharibi, Gorilla gorilla (Western gorilla)
- Ngagi wa Nijeria, Gorilla g. diehli (Cross River gorilla: Nijeria na Kameruni)
- Ngagi wa Uwanda wa Chini Magharibi, Gorilla g. gorilla (Western lowland gorilla: Kameruni, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Gaboni, Ginekweta, Kongo, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo na Angola)
- Ngagi Mashariki au Gorila Mashariki, Gorilla beringei (Eastern gorilla)
- Ngagi, Gorilla
- Hominini (Hominini)
- Sokwe Mtu, Pan
- Bonobo au Sokwe Mtu Mdogo, Pan paniscus (Bonobo au Pygmy chimpanzee: Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo)
- Sokwe Mtu wa Kawaida, Pan troglodytes (Common chimpanzee)
- Sokwe Mtu Mashariki, Pan t. schweinfurthii (Eastern chimpanzee: Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudani, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Uganda, Rwanda, Burundi, Tanzania na Zambia)
- Sokwe Mtu wa Kati, Pan t. troglodytes (Central chimpanzee: Kameruni, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ginekweta, Gaboni, Kongo na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo)
- Sokwe Mtu wa Nijeria, Pan t. vellerosus (Nigerian chimpanzee: Nijeria na Kameruni)
- Sokwe Mtu Magharibi, Pan t. verus (Western chimpanzee: Senegali, Mali, Gine, Sierra Leone, Liberia, Kodivaa na Ghana)
- Homo
- Binadamu, Homo sapiens
- Sokwe Mtu, Pan
- Gorillini
Spishi zilizokwisha
[hariri | hariri chanzo]- Ankarapithecus meteai (Mwisho wa Miocene ya Uturuki)
- Ardipithecus kadabba (Mwisho wa Miocene ya Uhabeshi)
- Ardipithecus ramidus (Mwanzo wa Pliocene ya Uhabeshi)
- Australopithecus afarensis (Pliocene ya Kenya, Tanzania na Uhabeshi)
- Australopithecus africanus (Pliocene ya Afrika Kusini)
- Australopithecus anamensis (Pliocene ya Kenya na Uhabeshi)
- Australopithecus bahrelghazali (Pliocene ya Chadi)
- Australopithecus garhi (Mwisho wa Pliocene ya Uhabeshi)
- Australopithecus sediba (Pleistocene ya Afrika Kusini)
- Gigantopithecus bilaspurensis (Mwisho wa Miocene ya Pakistani na Uhindi)
- Gigantopithecus blacky (Kati ya Pleistocene ya Uchina)
- Gigantopithecus giganteus (Pliocene ya Uhindi na Uchina)
- Kenyanthropus platyops (Kati ya Pliocene ya Kenya)
- Lufengpithecus chiangmuanensis (Miocene ya Uchina)
- Lufengpithecus keiyuanensis (Miocene ya Uchina)
- Lufengpithecus lufengensis (Miocene ya Uchina)
- Lufengpithecus yuanmouensis (Miocene ya Uchina)
- Nakalipithecus nakayamai (Mwisho wa Miocene ya Kenya)
- Oreopithecus bambolii (Miocene ya Italia na Afrika ya Mashariki)
- Orrorin tugenensis (Mwisho wa Miocene ya Kenya)
- Ouranopithecus macedoniensis (Mwisho wa Miocene ya Ugiriki)
- Paranthropus aethiopicus (Mwisho wa Pliocene ya Uhabeshi na Kenya)
- Paranthropus boisei (Pliocene na Pleistocene za Kenya na Tanzania)
- Paranthropus robustus (Pleistocene ya Afrika Kusini)
- Sahelanthropus tchadensis (Mwisho wa Miocene ya Chadi)
- Sivapithecus indicus (Kati ya Miocene ya Uhindi)
- Sivapithecus parvada (Kati ya Miocene ya Uhindi)
- Sivapithecus sivalensis (Kati ya Miocene ya Pakistani na Uhindi)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Sokwe Mtu (dume)
-
Bonobo (majike)
-
Ngagi-milima (dume)
-
Ngagi wa Uwanda wa Chini Mashariki (dume)
-
Ngagi wa Nijeria
-
Ngagi wa Uwanda wa Chini Magharibi (dume mzee)
-
Ngagi wa kike akivuka maji na kutumia fimbo kujishika
-
Orangutanu (wa Sumatra) ni sokwe aliyezoea miti zaidi
-
Orangutanu wa Borneo
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Sokwe (Hominidae) kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |