Majadiliano:Sokwe (Hominidae)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Asili ya "sokwere"[hariri chanzo]

Je, nani anajua ambapo neno hili "sokwere" linatoka? Nimelitafuta kila mahali, lakini linatajwa mara chache tu. Kwa kweli, takriban mikokoto yake yote inaelekea Kamusi ya Sayansi na Teknolojia. Neno hili haliwezi kuwa kosa la chapa? Nimeona makosa mengi kama hili katika kamusi. Nafikiri afadhali tafsiri ya "ape" iwe sokwe au nyani mkubwa. Ninapendekeza tafsiri zinazofuata:

  • chimpanzee – sokwe mtu au sokwemtu
  • gorilla – ngagi (jina linalotumika katika eneo lake la usambazaji; hii ni lugha ya Kingwana, lahaja ya Kiswahili)
  • orangutan – orangutanu
  • gibbon – giboni
(mchango wa mtumiaji:ChriKo)
Wazo zuri. Pia nimejaribu kufuatilia tafsiri ya viumbe hivi nimeona kwenye kamusi yangu inataja wote jina moja tu, basi. Tazama mifano ya maneno uliyoyataja hapo juu:
  1. gibbon n sokwe
  2. chimpanzee/chimp n sokwe
  3. gorilla n sokwe
  4. orangutan - kwenye kamusi yangu hakuna

Tabu au shida ya tafsiri hizi ni kwamba wao watu wa TUKI wametafsiri maana moja hao masokwe. Sidhani kama wote ni sawa (sijui kitu) - kazi kwako bwana ChriKo. Tafutia jina ambao unaona linafaa.--MwanaharakatiLonga 06:20, 24 Juni 2010 (UTC)

Nakubali pendekezo la "sokwe" kwa watu na nyani za hominidi. (BTW: hominidi = Hominoidea?)

Nisipokosei kuna watu huko kwenye taasisi ya TUKI na kamati ya KAST wanaoamua pekee yao au labda baada ya kupitishi orodha ya mapendekezo kwa kamati ndogo. Yaani kutoa kamusi kama KAST ni kazi gumu kwa sababu mambo mengi hayakujadiliwa kwa Kiswahili bado; labda wamekuta neno fulani baada limebuniwa na kutumiwa mara moja-au chache tu kimaandishi katika maandishi labda ya mtummoja tu. Labda wanaona wajaze nafasi katika orodha ya maeno yanayotakiwa kupata jina la Kiswahili wakiamua pekee yao.

Hata hivyo naona ni afadhali tukisimama kimsingi upande wa kamusi za TUKI lakini hapa naona sawa kwenda kando kidogo.

Hapo mimi naona kazi yetu ni muhimu maana sisi tunapeleka maneno katika uwanja wa umma wa wasemaji wa Kiswahili tofauti na maandishi katika gazeti la kisayansi inayolala katika maktaba ya chuo kikuu sijui wapi na kufikia wasomaji wangapi? --Kipala (majadiliano) 07:49, 24 Juni 2010 (UTC)

Afadhali na wewe mzee wangu ulivyoliona hili. Nikirejea ujumbe wa Oliver kuhusu kutowatupa mkono wataalamu wa lugha, ilinishinda kutumia bunilizi ya kinjozi kwa sababu inapishana na sauti ya kutamka maneno ya namna hiyo. Nilipinga na kuona kwamba FANTASY afadhali iwe: ubunifu wa kinjozi. LAKINI kwa kuwa kuna mtu mmoja kapendekeza vile ajisikiavyo yeye, basi imepita, lakini nitaendelea kubisha. Pia, hao watu wa TUKI mara nyingi hubadili maneno mara kwa mara. Hii inaashiria ya kwamba hawana uhakika na kile wanachokifanya. Pia, hawapatikani na wala hawashauriki. Wana kipindi katika Redio One, lakini hawatoi mapendekezo kwa wananchi angalau wachingie na wasikie mawazo kutoka kwa watu wengine. Ikiwa wana-kipindi, basi ni rahisi kuomba mawazo kutoka kwa watu angalau ingeboresha lugha yetu. Watu wa EAT tunaita "UKIRITIMBA" wa watu fulani wanaojiona wao zaidi ya raia milioni 43. Kazi ipo!--MwanaharakatiLonga 09:23, 24 Juni 2010 (UTC)
Asante sana, marafiki, kwa mawazo yenu. Sitaki kupuuza maoni ya wataalamu wa lugha, lakini inaonekana kama hawana maoni ya pamoja juu ya jambo hili, na zaidi ya hiyo hawa si wataalamu wa wanyama. Spishi za sokwe si moja tu, kwa hivyo jina moja halifai. Ninadumisha mapendekezo yangu na pia ningependa kusogeza ukurasa huu, kwa sababu sipendi vichwa kwa lugha za kigeni (hata vikiwa vimeswahilishwa). Msipokuwa na kauli nyingine nitaendelea. ChriKo (majadiliano) 23:25, 24 Juni 2010 (UTC)
Kwa upande wangu sina kauli. Sijui wenzi-wangu. Endelea bwana!--MwanaharakatiLonga 06:06, 25 Juni 2010 (UTC)
Sawa kabisa. --Kipala (majadiliano) 10:10, 26 Juni 2010 (UTC)