Saba abati

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha takatifu ya karne za kati ya Mt. Saba.

Saba Abati (Mutalaska, karibu na Caesarea Mazaca, Kapadokia, leo nchini Uturuki, 439Yerusalemu, leo nchini Israeli/Palestina, 532), alikuwa mmonaki padri aliyeanzisha monasteri kadhaa, ambazo kati yake maarufu zaidi ni ile yenye jina lake (Mar Saba).[1]

Tangu kifo chake anaheshimiwa na Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 5 Desemba[2].

Jina[hariri | hariri chanzo]

Jina hilo linatokana na neno la Kiaramu סַבָּא (sabba') lenye maana ya "mzee".[3]

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Alipokuwa na umri wa miaka minane, Saba alipelekwa katika monasteri ya Aleksandria (Misri) akawa mtaalamu wa Biblia.

Baadaye alikataa agizo la wazazi la kutoka utawani ili kuoa.

Baadaye tena alihamia monasteri nyingine za Yerusalemu.

Kisha kufikia miaka thelathini, alipewa baraka ya abati Eutimio Mkuu ajitenge na wote akaishi kama mkaapweke katika pango, isipokuwa Jumamosi alipokuwa anarudi kwa wenzake kushiriki ibada na mlo.

Baada ya muda aliruhusiwa kutorudi Jumamosi, akawa peke yake kabisa miaka mitano, chini ya uongozi wa Eutimio. Kwa kuona ukomavu wake, huyo alianza kumchukua naye kwenda porini kila mwaka tangu tarehe 14 Januari hadi Jumapili ya Matawi.

Eutimio alipofariki (473 hivi), Saba alihamia pango lingine tena, mbali na monasteri.

Huko katika Bonde la Kidron, kusini kwa Yerusalemu, walianza kukusanyika wafuasi kadhaa hata ikatokea monasteri kuu yenye jina lake (484).

Baadhi yao walipoanza kumpinga akidai abati awe padri, alihamia kusini, karibu na Thekoa.

Patriarki Salustius wa Yerusalemu alimpa upadrisho mwaka 491 na kumteua abati mkuu wa monasteri zote za Palaestina Prima mwaka 494.

Alipinga kabisa mafundisho ya Wamonofisiti na ya wafuasi wa Origen, hata akaenda Konstantinopoli mwaka 511 na mwaka 531 kumhimiza kaisari Anastasio I dhidi yao[4].

Saba alitunga kanuni ya kimonaki ya kwanza kwa ibada za kanisani (Jerusalem Typikon) za monasteri zote za mapokeo ya Kigiriki.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Sabbas' Life was written by his disciple Cyril of Scythopolis. The chief modern authority is A. Ehrhard in Wetzer and Welte's Kirchenlexikon (ed. 2) and Römische Quartalschaft, vii; see also Pierre Helyot, Histoire des ordres religioux (1714), i.C.16, and Max Heimbucher, Orden u. Kongregationen (1907), i, §10.
  2. Martyrologium Romanum
  3. "Sabas". Origin of names. 
  4. "St. Sabbas". Catholic Encyclopedia. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.