Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira (Tanzania)
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira | |
---|---|
Mamlaka | Tanzania |
Makao Makuu | Makore area, Dodoma |
Waziri | January Makamba |
Naibu Waziri | Kangi Alphaxard Lugola |
Tovuti | vpo.go.tz |
Muungano na Mazingira ni wizara kamili ambayo ipo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania: kwa hivyo Waziri wake anaitwa waziri wa Nchi Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira.
Kimsingi Makamu wa Rais huendelea na majukumu yake ya umakamu wa Rais na hivyo yeye kuwa ni msimamizi tu wa wizara hii ambayo mojawapo ya majukumu yake ni kuratibu shughuli za muungano na mazingira chini ya Waziri mwenye dhamana pamoja na Naibu Waziri. Hao ndio wasimamizi wa Wizara hiyo. Hivyo hii ni wizara miongoni mwa Wizara za Serikali ya Tanzania.[1]
Ofisi kuu za wizara hii zilikuwa jijini Dodoma.
Tarehe 7 Oktoba 2017 Rais John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa awamu ya tano, alifanya mabadiliko kidogo katika Wizara mbalimbali na kuwabadilisha baadhi ya mawaziri na manaibu waziri na katika mabadiliko hayo wapo pia Mawaziri wapya walioingia na manaibu Waziri wapya, ikiwepo hii ya mazingira ambapo aliteuliwa Naibu Waziri na mnamo tarehe 9 Oktoba 2017 aliweza kuwaapisha rasmi, akiwemo naibu Waziri wa Mazingira.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-07-21. Iliwekwa mnamo 2018-06-17.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti Archived 30 Januari 2018 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |