Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira (Tanzania)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira
MamlakaTanzania
Makao MakuuMakore area, Dodoma
WaziriJanuary Makamba
Naibu WaziriKangi Alphaxard Lugola
Tovutivpo.go.tz

Muungano na Mazingira ni wizara kamili ambayo ipo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania: kwa hivyo Waziri wake anaitwa waziri wa Nchi Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira.

Kimsingi Makamu wa Rais huendelea na majukumu yake ya umakamu wa Rais na hivyo yeye kuwa ni msimamizi tu wa wizara hii ambayo mojawapo ya majukumu yake ni kuratibu shughuli za muungano na mazingira chini ya Waziri mwenye dhamana pamoja na Naibu Waziri. Hao ndio wasimamizi wa Wizara hiyo. Hivyo hii ni wizara miongoni mwa Wizara za Serikali ya Tanzania.[1]

Ofisi kuu za wizara hii zilikuwa jijini Dodoma.

Tarehe 7 Oktoba 2017 Rais John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa awamu ya tano, alifanya mabadiliko kidogo katika Wizara mbalimbali na kuwabadilisha baadhi ya mawaziri na manaibu waziri na katika mabadiliko hayo wapo pia Mawaziri wapya walioingia na manaibu Waziri wapya, ikiwepo hii ya mazingira ambapo aliteuliwa Naibu Waziri na mnamo tarehe 9 Oktoba 2017 aliweza kuwaapisha rasmi, akiwemo naibu Waziri wa Mazingira.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-07-21. Iliwekwa mnamo 2018-06-17. 

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]