January Makamba
Mandhari
| January Makamba MB | |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki | |
| Muda wa Utawala 1 Septemba 2023 – 21 Julai 2024 | |
| Rais | Samia Suluhu |
|---|---|
| mtangulizi | Stergomena Tax |
| aliyemfuata | Mahmoud Kombo |
Waziri wa Nishati | |
| Muda wa Utawala 12 Septemba 2021 – 31 Agosti 2023 | |
| Rais | Samia Suluhu |
| mtangulizi | Medard Kalemani |
| aliyemfuata | Doto Biteko |
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais | |
| Muda wa Utawala 12 Desemba 2015 – 21 Julai 2019 | |
| Rais | John Magufuli |
| Waziri Mkuu | Kassim Majaliwa |
| aliyemfuata | George Simbachawene |
Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia | |
| Muda wa Utawala 7 Mei 2012 – 5 Novemba 2015 | |
| Rais | Jakaya Kikwete |
| mtangulizi | Charles Kitwanga |
| Muda wa Utawala November 2010 – October 2025 | |
| mtangulizi | William Shellukindo |
| tarehe ya kuzaliwa | 28 Januari 1974 Singida, Tanzania |
| chama | CCM |
| ndoa | Ramona Urassa |
| mahusiano | Yusuf Makamba (Baba) |
| watoto | 2 |
| makazi | Dar es Salaam |
| mhitimu wa | St. John’s University George Mason University |
| tovuti | januarymakamba.com |
January Makamba (alizaliwa 28 Januari 1974) ni mwanasiasa na Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi. Anawakilisha Jimbo la Bumbuli, katika wilaya ya Lushoto, mkoa wa Tanga.
Alifaulu katika uchaguzi mkuu wa tarehe 31 Oktoba 2010 bila mpinzani kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi. Mwaka 2015 alijaribu kupata nafasi ya mgombea wa urais kwa chama cha CCM [1]. Alirudi kwenye bunge 2015 na 2020 tena bila kuchaguliwa akiwa mgombea pekee.
Chini ya rais John Pombe Magufuli aliwahi kuwa Waziri wa Mazingira (2016-2019). Mwaka 2021 alipata kuwa waziri wa nishati katika baraza la mawaziri chini ya rais Samia Suluhu Hassan[2].
Marejeo
- ↑ http://taifaletu.blogspot.com/2015/06/hotuba-ya-january-makamba-ya-kutangaza.html Hotuba ya January Makamba ya kutangaza kuomba nafasi ya Urais wa Tanzania, Juni 7, 2015.
- ↑ https://greenwavesmedia.co.tz/sw/2021/09/makamba-aanza-kazi-rasmi-wizara-ya-nishati/ MAKAMBA AANZA KAZI RASMI WIZARA YA NISHATI, greenwavesmedia 13 Septemba 2021
