Nenda kwa yaliyomo

Mwinjili Luka

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mwinjilisti Luka)
Luka akimchora kwa mara ya kwanza Bikira Maria, kielelezo cha imani katika Injili yake.
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
Yesu
Yesu Kristo na Ukristo

Umwilisho   Utoto wa Yesu   Ubatizo   Arusi ya Kana   Utume wa Yesu   Mifano ya Yesu   Miujiza ya Yesu   Kugeuka sura   Karamu ya mwisho   Msalaba wa Yesu   Maneno saba   Kifo cha Yesu   Ufufuko wa Yesu   Kupaa mbinguni   Ujio wa pili  Yesu na matabiri ya Agano la Kale   Injili   Majina ya Yesu katika Agano Jipya   Yesu kadiri ya historia   Tarehe za maisha ya Yesu   Kristolojia

Mazingira ya Yesu

Wayahudi   Kiaramu   Bikira Maria   Yosefu (mume wa Maria)   Familia takatifu   Ukoo wa Yesu   Ndugu wa Yesu   Yohane Mbatizaji

Mitazamo juu ya Yesu

Mitazamo katika Agano Jipya  · Mitazamo ya Kikristo   Mitazamo ya Kiyahudi   Mitazamo ya Kiislamu   Yesu katika sanaa

Mwinjili Luka (kwa Kigiriki Λουκᾶς, Lukas) ni Mkristo wa karne ya 1 ambaye tangu zamani za Mababu wa Kanisa anasadikiwa kuwa mwandishi wa Injili ndefu kuliko zote za Biblia ya Kikristo. Humo alisimulia kwa ufasaha na kupanga kwa utaratibu mzuri matendo na mafundisho ya Yesu, akastahili kuitwa "mwandishi wa upole wa Kristo" (Dante Alighieri)[1].

Vilevile anasadikiwa kuwa mwandishi wa kitabu cha Matendo ya Mitume kinachoendeleza Injili hiyo ili kuonyesha kazi ya Yesu Kristo ilivyoendelea katika Kanisa lake kwa nguvu ya Roho Mtakatifu hadi mwaka 63 BK.

Hivyo Luka, mtunzi pekee wa Agano Jipya asiye Myahudi, anahesabiwa kuwa ameandika robo ya sehemu hiyo ya pili ya Biblia nzima ya Ukristo.

Pamoja na Wakristo wengine wengi, Kanisa Katoliki linamheshimu kama mtakatifu na msimamizi wa madaktari hasa katika sikukuu yake, tarehe 18 Oktoba[2].

Luka alizaliwa katika familia ya Kiyunani, labda mjini Antiokia ya Syria, leo nchini Uturuki.

Inasadikiwa aliongozwa na Mtume Paulo kumpokea Yesu na alifanya naye kazi kwa takribani miaka 18. Pamoja na ukaribu huo, hata hivyo hakuandika tu mitazamo ya Paulo, hii ni kuonesha kuwa aliyaandika yale aliyovuviwa na Roho Mtakatifu baada ya utafiti wa kihistoria katika vyanzo mbalimbali.

Anatajwa na Paulo katika barua zake kama mganga aliye jirani naye katika majaribu yake: Waraka kwa Filemoni, mstari 24; Waraka kwa Wakolosai 4:14 na Waraka wa pili kwa Timotheo 4:11.

Uaminifu huo wa Luka kwa Paulo unalingana na habari za Matendo ya Mitume, ambapo Luka hajitaji, lakini anasimulia safari za Paulo akitumia mara nyingi neno "sisi". Hivyo anajishuhudia kuwa mshiriki wa utume wake.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Marejeo ya Kiswahili

[hariri | hariri chanzo]
  • John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 362-363
  • Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 320
  • Maurice Soseleje, Kalendari yetu – Maisha ya Watakatifu – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Peramiho 1986 – ISBN 9976-63-112-X, uk. 81

Marejeo ya lugha nyingine

[hariri | hariri chanzo]
  • I. Howard Marshall. Luke: Historian and Theologian. Downers Grove, Illinois: InterVarsity Press.
  • F.F. Bruce, The Speeches in the Acts of the Apostles. London: The Tyndale Press, 1942. Ilihifadhiwa 31 Mei 2012 kwenye Wayback Machine.
  • Helmut Koester. Ancient Christian Gospels. Harrisburg, Pennsylvania: Trinity Press International, 1999.
  • Burton L. Mack. Who Wrote the New Testament?: The Making of the Christian Myth. San Francisco, California: HarperCollins, 1996.
  • J. Wenham, "The Identification of Luke", Evangelical Quarterly 63 (1991), 3–44

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwinjili Luka kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.