Magdalena wa Canossa
Magdalena wa Canossa (Verona, Italia, 1 Machi 1774 - Verona, 10 Aprili 1835) alikuwa mwanamke aliyejinyima utajiri wake wote akaanzisha mashirika ya Mabinti wa Upendo (Wakanosa) na Wana wa Upendo (Wakanosa) kwa ajili ya malezi ya Kikristo ya vijana.
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu mwaka 1988.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[1].
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Utoto
[hariri | hariri chanzo]Alizaliwa na sharifu Ottavio wa Canossa na mke wake Teresa Szluha, akiwa mtoto wa tatu kati ya sita.
Mwaka 1779 baba alifariki ghafla, na miaka miwili baadaye mama aliolewa tena na Edoardo Zenetti wa Mantova.
Magdalena na watoto wenzake walikabidhiwa kwa walezi wasomi: padri Pietro Rossi kwa mtoto wa kiume, na Fransiska Mariana Capron kwa wale wa kike. Huyo mama kutoka Ufaransa aliharibu kwa ukali wake, lakini alipoacha kazi, Magdalena alipatwa ghafla na ugonjwa mbaya.
Wito
[hariri | hariri chanzo]Alipopona, Magdalena alimshirikisha padri Pietro Rossi uamuzi wake wa kujitoa kwa Mungu akaanza kupitia sheria za mashirika mbalimbali.
Ndipo alipojiunga na monasteri ya Wakarmeli Peku ya Verona, tarehe 2 Mei 1791, lakini baada ya miezi kumi alitambua ana wito tofauti, si ule wa kuishi daima ndani ya ugo.
Chini ya padri Luigi Libera alichunguza wito wake maalumu tangu mwaka 1792 hadi 1799 na hatimaye alikutana na askofu Andrea Avogadro wa Verona ili kupendekeza bila mafanikio mpango wake wa matendo ya huruma.
Wakati huo ilimbidi Magdalena kusimamia familia yake pamoja na mali yake, lakini alitekeleza ndoto yake ya kukusanya wasichana wasio na nyumba na kutembelea hospitali.
Kati ya 1802 na 1808 aliishi kidogo katika nyumba ya familia na kidogo katika nyumba alizozikodi kwa ajili ya wasichana hao.
Mwanzilishi
[hariri | hariri chanzo]Tarehe 8 Mei 1808 aliweza kushinda upinzani wa wanafamilia akahamia kati ya wasichana wake na kuanzisha shirika la kike ili kushughulikia mahitaji ya jamii kupitia shule, katekesi, ziara hospitalini na malezi ya walimu wa vijijini.
Kati ya mwaka 1808 na 1835, Magdalena alisafiri sana na kuandika barua nyingi ili kuthibitisha kazi yake na kupata kibali, pamoja na kuanzisha jumuia nyingine sehemu mbalimbali za Italia.
Mwaka 1819 shirika lilikubaliwa halafu Papa Leo XII alithibitisha katiba yake kwa hati Si nobis 23 Desemba 1828.
Mpango wa kuanzisha tawi la kiume, aliokuwanao tangu mwaka 1799, ulitekelezeka mwaka 1831 tu huko Venezia.
Magdalena alifariki huko Verona tarehe 10 Aprili 1835.
Maandishi
[hariri | hariri chanzo]Kumbukumbu
[hariri | hariri chanzo]Zinatunzwa kumbukumbu zake alizoziandika kwa agizo la mwakilishi wa Papa na kwa kutumia nafsi ya tatu: zinafikia hadi mwaka 1827 lakini kwa kuruka miaka 1816 hadi 1824.
Barua
[hariri | hariri chanzo]Ziko bado 3,000 zilizokusanywa na Emilia Dossi kati ya mwaka 1976 na 1983:
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Vyanzo
[hariri | hariri chanzo]- Maddalena di Canossa, Epistolario, a cura di Emilia Dossi, 8 volumi, Pisani, Isola del Liri 1977-1983.
- Maddalena di Canossa, Regole e scritti spirituali, a cura di Emilia Dossi, 2 volumi, Pisani, Isola del Liri 1984-1985.
- Maddalena di Canossa, Memorie, Rusconi, Milano 1988.
- Libera Luigi, Lettere di direzione spirituale alla marchesina Maddalena Gabriella di Canossa, a cura di Cattari A., IPL, Milano 1982.
- Bresciani C., Vita di Maddalena marchesa di Canossa, Vicentini e Franchini, Verona 1849.
- Piccari T., Sola con Dio solo. Memorie di Maddalena di Canossa, Ancora, Milano 1966.
- Cattari A., Maddalena Gabriella di Canossa, IPL, Milano 1984.
- Farina M. - Rispoli F., Maddalena di Canossa, SEI, Torino 1995.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti ya Wakanosa Ilihifadhiwa 19 Aprili 2014 kwenye Wayback Machine.
- Tovuti ya Wakanosa Wanawake Ilihifadhiwa 6 Aprili 2022 kwenye Wayback Machine.
- Tovuti ya Wakanosa Wanaume Ilihifadhiwa 14 Mei 2021 kwenye Wayback Machine.
- Maelezo ya Vatikani kwa siku ya kumtangaza mtakatifu
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |