Jokate Mwegelo
Jokate Mwegelo | |
---|---|
Amezaliwa | 20 Machi 1987 |
Utaifa | Mtanzania |
Majina mengine | Jojo Kidoti |
Mhitimu | Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (Shahada ya Sayansi ya Siasa) |
Kazi yake | mwigizaji, mjasiriamali, mtangazaji, mwimbaji, mwanasiasa |
Miaka ya kazi | 2006-hadi sasa |
Jokate Mwegelo (alizaliwa 20 Machi 1987) ni mwigizaji wa filamu, mjasiriamali na mwanasiasa kutoka nchini Tanzania. Mnamo mwezi Julai 2018 aliteuliwa na rais John Magufuli kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe.
Mnamo mwaka 2006 alifanikiwa kushika nafasi ya pili katika shindano la Miss Tanzania akiwa nyuma ya Wema Sepetu ambaye alishika nafasi ya kwanza [1]
Jokate vilevile alikuwa mtangazaji na mwimbaji[2][3][4][5] na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Kidoti Company.[6][7]
Mwaka 2011, alishinda tuzo ya Zanzibar International Film Festival kama mwigizaji bora wa kike.[8].Mwaka 2017, Mwegelo aliingizwa katika jarida la Forbes katika Forbes 30 Under 30 kutoka Afrika.[9]
Maisha ya awali na elimu
[hariri | hariri chanzo]Jokate Mwegelo alizaliwa jijini Washington, D.C., Marekani, ambapo wakati huo wazazi wake walikuwa wanafanya kazi.
Alikulia jijini Dar es Salaam, Tanzania. Alianza elimu ya msingi katika shule ya Olympio Primary School na baadaye St. Anthony High School, halafu Loyola High School, Dar es Salaam.
Alihitimu katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, ambapo alipata shahada ya sayansi ya siasa na falsafa.
Miss Tanzania 2006
[hariri | hariri chanzo]Alikuwa mshindi wa pili katika shindano la Miss Tanzania mwaka 2006.[10] Vilevile alipewa jina la balozi wa Redds fashion na balozi wa gazeti la Citizen, baada ya kupata kura nyingi mwaka huo.[5]
Kabla ya Miss Tanzania, alishindana katika Miss Kurasini 2006, shindano ambalo alishinda, kisha kuelekea juu zaidi na kuwa Miss Temeke 2006, ambako pia alishinda.[11]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 2018 aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania John Joseph Magufuli kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe, mwaka 2020 alibadilishwa na kuwa mkuu wa wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Kuigiza
[hariri | hariri chanzo]Mwaka wa 2007, alipata kucheza filamu yake ya kwanza iliyojulikana kwa jina la Fake Pastors, akiwa na Vincent Kigosi, Lisa Jensen, mshindi wa tatu wa Miss Tanzania 2006 na marehemu Adam Kuambiana.[12]
Mwaka wa 2008, amecheza katika filamu ya From China With True Love[13]
Mwaka2010, alionekana katika filamu ya Chumo, filamu iliyoandaliwa na Media for Development International, kuhusu elimu juu ya ugonjwa wa malaria.[14] Filamu hii ilimwezesha kupata tuzo ya Zanzibar International Film Festival akiwa kama mwigizaji bora wa kike kwa mwaka 2011 na kuchaguliwa kama mwigizaji wa Pan-Afrika katika tuzo za 2012 Nigeria Entertainment Awards.
Vilevile amepata kuonekana katika mfululizo wa tamthilia maarufu kwa jina Siri Ya Mtungi, iliokua imendaliwa na Jordan Riber na kuongozwa na Karabani, mnamo mwaka 2013.[15] Mwaka wa 2014, amecheza uhusika wa "Ndekwa" katika filamu ya Mikono Salama, ambayo ilimpelekea apate tuzo nyingine ya Zanzibar International Film Festival akiwa mwigizaji bora wa kike kwa filamu za Kiswahili.[16]
Kampuni ya Kidoti
[hariri | hariri chanzo]Muziki
[hariri | hariri chanzo]Alishirikishwa katika wimbo wa Japo Nafasi wa Cpwaa akiwa na A.Y. katika wimbo wa Kings and Queen, na Amani, kutoka Kenya. Mwaka wa 2013, alitoa wimbo wake akiwa na Lucci, uliyoitwa 'Kaka na Dada.[17][18] Mwaka wa 2015, akadondosha wimbo wake mwingine uliyoitwa Leo akiwa na mwimbaji mwingine kutoka nchini Nigeria maarufu kama Ice Prince.[19]
Siasa
[hariri | hariri chanzo]Jokate hakujulikana kujishughulisha na siasa hadi mwaka 2017 alipoteuliwa na Umoja wa Vijana wa chama cha CCM (UVCCM) kuongoza Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi ya umoja huu akiwa kaimu katibu wa idara hii. Yeye mwenyewe alitaja maarifa ya utoto wake alipohamasishwa na bibi yake aliyekuwa mwasisi wa Umoja wa Walimu Tanzania katika Mkoa wa Rukwa kuona ni muhimu kujitoa katika jamii na kuchukua nafasi za uongozi. [20] Wakati ule magazeti yalileta taarifa kuwa uteuzi wake ulipingwa na sehemu ya viongozi wa umoja huu.[21]
Kwenye mwezi wa Machi 2018 aliondolewa katika nafasi hii kwa azimio la kamati kuu ya UVCCM.[22]
Mwisho wa mwezi wa Julai 2018 aliteuliwa na rais Magufuli kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe[23], uteuzi ambao ulileta cheche nyingi katika uwanja wa mitandao nchini Tanzania. Wapo waliobeza uteuzi huo, wapo waliosifia. Wengine waliweka picha zake za zamani zilizokuwa hazina maadili ili kukebehi uteuzi huo.
Filamu
[hariri | hariri chanzo]- Movies
Mwaka | Filamu | Uhusika | Washiriki |
---|---|---|---|
2007 | Fake Pastors[24] | Jackie | Vincent Kigosi, Adam Kuambiana, Lisa Jensen na Ahmed Ulotu |
2008 | From China With Love [25] | Vincent Kigosi, Blandina Chagula, Suzan Lewis na Aileen Francisco | |
2011 | Chumo[26] | Amina | Yusuph Mlela, Hussein Mkiety (Sharobaro) |
2014 | Mikono Salama[27] | Ndekwa | Jacob Steven, Single Mtambalike na Irene Uwoya |
- Mfululizo wa TV
Mwaka | Mfululizo | Uhusika | Maelezo |
---|---|---|---|
2013-2014 | Siri Ya Mtungi Msimu wa 2[28] | Mwanamitindo |
Diskografia
[hariri | hariri chanzo]- 2013
Kaka Dada akiwa na Lucci
- 2015
Leo Leo akiwa Ice Prince
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "JOKATE:Afikiria kubadili fani akiacha urembo". Mwananchi (kwa Kiingereza). 2021-03-15. Iliwekwa mnamo 2024-08-02.
- ↑ YManager (20 Agosti 2016). "'I keep pushing myself so I will leave a mark...' - Leading Ladies Africa speaks to Jokate Mwegelo of Kidoti - YNaija". Iliwekwa mnamo 6 Septemba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Joketi Mwegelo - Actor, Model, Singer, — Bongo Movies". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-09-21. Iliwekwa mnamo 6 Septemba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Channel O VJ: Jokate - Channel O TV Online". 17 Oktoba 2011. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-01-26. Iliwekwa mnamo 6 Septemba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 5.0 5.1 "Happy Birthday Jokate Mwegelo ( watch video + her Biography inside) - Bongo5.com". Iliwekwa mnamo 6 Septemba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "BongoToday.com - Entertainment and Lifestyle : Kidoti partners with Rainbow Shell Craft Company from China". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-09-21. Iliwekwa mnamo 6 Septemba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "VJ Blog: KidOti - Define Your Beauty - Channel O TV Online". 24 Mei 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-01-26. Iliwekwa mnamo 6 Septemba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ http://www.africultures.com/php/index.php?nav=murmure&no=7524
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-09-21. Iliwekwa mnamo 2017-09-12.
- ↑ Blog, Michuzi (6 Agosti 2006). "MICHUZI BLOG: miss tz 2006". Iliwekwa mnamo 6 Septemba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Blog, Michuzi (25 Juni 2006). "MICHUZI BLOG: miss temeke 2006". Iliwekwa mnamo 6 Septemba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Fake Pastors — Bongo Movie - Tanzania". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-07-04. Iliwekwa mnamo 6 Septemba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "From China With Love — Bongo Movie - Tanzania". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-07-04. Iliwekwa mnamo 6 Septemba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Chumo Home". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-05-27. Iliwekwa mnamo 6 Septemba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Saleem, Trim (25 Novemba 2013). "SWP: BEHIND THE SCENES: JOKATE, MONALISA AND RICHA ADHIA IN SIRI YA MTUNGI SEASON 2". Iliwekwa mnamo 6 Septemba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "ZIFF 2015: The winners". 26 Julai 2015. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-06-10. Iliwekwa mnamo 6 Septemba 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ http://www.bongo5.com/picha-jokate-na-lucci-ni-kaka-na-dada-tu-08-2013/
- ↑ http://www.bongo5.com/photos-jokate-and-lucci-to-release-their-long-awaited-surprise-tonight-08-2013/
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-01-26. Iliwekwa mnamo 2017-09-12.
- ↑ "JOKATE: UVCCM LAZIMA IBADILIKE KUANGALIA CHANGAMOTO ZA VIJANA". mtanzania.co.tz ya tarehe Jun 28th, 2017. Iliwekwa mnamo 2018-07-30.
- ↑ "JOKATE AIVURUGA UVCCM". mtanzania.co.tz ya tarehe 24 Aprili 2017. Iliwekwa mnamo 2018-07-30.
- ↑ "SABABU ZA KUTUMBULIWA JOKATE ZATAJWA". mtanzania.co.tz ya tarehe 25 MAchi 2018 (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2018-07-30.
- ↑ "Jokate, Kafulila, Katambi among loyalists Magufuli rewards in", The Citizen ya tarehe 30 Julai 2018 (kwa Kiingereza), 2018-07-29, iliwekwa mnamo 2018-07-30
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-07-04. Iliwekwa mnamo 2017-09-12.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-07-04. Iliwekwa mnamo 2017-09-12.
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-01-08. Iliwekwa mnamo 2017-09-12.
- ↑ http://www.bongo5.com/video-trailer-ya-mikono-salama-aliyocheza-jokate-jb-uwoya-na-richie-01-2014/
- ↑ http://www.bongo5.com/jokate-kuigiza-kwenye-msimu-wa-pili-wa-tamthilia-ya-siri-ya-mtungi-11-2013/
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Jokate Mwegelo at the Internet Movie Database
- PROFILE: A-Z Jokate Kuzaliwa Marekani, Elimu,Miss Tz, Hadi U-DC
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jokate Mwegelo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |