Wema Sepetu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Wema Abraham Sepetu (amezaliwa 28 Septemba 1988) ni mwanamitindo, mjasiriamali na mwigizaji kutoka nchini Tanzania.

Aliwahi kuwa Miss Tanzania kwa mwaka wa 2006.

Maisha ya awali, elimu, na sanaa[hariri | hariri chanzo]

Wema ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto wanne wa Abraham Sepetu. Alianza elimu ya msingi na hadi sekondari amesomea katika shule moja tu iitwayo "Academic International" iliyopo maeneo ya Mikocheni, Dar es Salaam. Pamoja na yote hayo, binti huyu amelelewa na kuishi kama mtu wa Magharibi (Ulaya).

Kipaji zaidi cha Wema kiligundulika katika sanaa ya filamu, ambapo alifanikiwa kucheza vema kabisa katika filamu A Point of No Return akishirikiana na mchezaji filamu maarufu wa Kitanzania Steven Kanumba.

Wema alivishwa pete ya uchumba na msanii maarufu wa Bongo Flava Diamond, lakini kwa sasa wameshaachana.

Pia Wema amekuwa akijulikana kwa kuwa na sauti ndogondogo.

Baadhi ya filamu za Wema[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]