Nenda kwa yaliyomo

Lisa Jensen

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lisa Jensen
AmezaliwaLisa Jensen
27 Aprili 1988 (1988-04-27) (umri 36)
UtaifaMTanzania
Kazi yakeMwigizaji, mjasiriamali, mtangazaji, mwimbaji
Miaka ya kazi2006-hadi sasa

Lisa Jensen (amezaliwa tar. 27 Aprili, 1988) ni mwanamitindo na mwigizaji kutoka nchini Tanzania. Lisa alipata kushiriki katika shindano la Miss Tanzania 2006 na kuibuka mshindi wa tatu, huku sehemu ya kwanza ikinyakuliwa na Wema Sepetu na ya pili Jokate Mwegelo. Katika upande wa filamu alianza kutambulika sana baada ya kucheza katika filamu Fake Pastors ya mwaka 2007 akiwa na Jokate, Vincent Kigosi na Adam Kuambiana. Mwaka wa 2012, alishinda Miss Redds Tanzania na kwenda kushiriki katika mashinda ya dunia yaliyofanyika huko nchini China mwaka 2013. [1]

Filmografia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
  1. Lisa Jense Ilihifadhiwa 27 Juni 2017 kwenye Wayback Machine. katika Bongo Cinema.com