Adam Kuambiana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Adam Kuambiana
Amezaliwa Adam Philip Kuambiana
(1976-06-06)Juni 6, 1976 Iringa, Tanzania
Amekufa Mei 17, 2014 (umri 37) Dar es Salaam, Tanzania
Kazi yake Mwigizaji, mtunzi, mtayarishaji, mwongozaji
Miaka ya kazi Miaka ya 2000 - 2014

Adam Philipo Kuambiana (6 Juni 1976 - 17 Mei, 2014) alikuwa msanii wa maigizo na mtayarishaji na mwongozaji wa filamu kutoka nchini Tanzania. Anajulikana sana kwa uhusika wake katika filamu ya Fake Pastors (2007), Mr. Kadamanja (2014), Chaguo Langu (2012), vilevile katika Aliyemchokoza Kaja, Danija, Faith More Fire, Bad Luck, Scola, The Boss, Mr. Nobody, Radhi ya Mke, Lost Sons, My Fiance, Jesica, Life of Sandra, Basilisa, My Flower, Regina, Born Again, na It's Too Late.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Kuambiana alizaliwa tarehe 6 Juni 1976 huko Ifunga mkoa wa Iringa. Alipata elimuya msingi katika shule ya Mlimani Jijini Dar halafu baadaye elimu ya sekondari katika shule ya Tambaza na hatimaye kuhamia jijini Nairobi ambapo alienda kumalizia kidato cha tano nasita kisha akaenda Afrika Kusini kupata elimu ya filamu. Elimu hiyo iliyomwezesha katika kuongoza na kuandika miaswada andishi kadhaa ya filamu za Tanzania.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Adamu Kuambiana amepata kuoneakana katika filamu mbalimbali, lakini umaarufu wake hasa ulianza mwaka wa 2007 baada ya kucheza katika filamu ya Fake Pastors, ambamo humo alionesha uwezo wa hali ya juu. Filamu inatokana na kitabu kilichotungwa na Eric Shigongo. Kazi ya kuongoza filamu alianza baada ya kujiunga na RJ Company inayomilikiwa na Vincenti Kigosi na Blandina Changula. Filamu nyingi alifanya akiwa na Jerusalem Film Co. chini ya Jacob Stephen lakabu JB.

Kifo[hariri | hariri chanzo]

Taarifa za kufa kwake zilianza kuvuma siku ya 17 Mei, 2014. Huku ripoti ya polisi ikionesha sababu zilizopelekea kufa kwa Adam Kuambiana ni vidonda vya tumbo na unywaji mwingi wa pombe bila kula. [1] Vilevile kukatokea na dhana kibao huenda mareheu aliwekewa sumu katika vinywaji na kadhalika.[2][3]

Baadhi ya filamu zilizochaguliwa[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Jestina George na habari za SABABU ZA KIFO CHA ADAM KUAMBIANA ZATAJWA.
  2. Mzito kuhusu kifo cha Adam Kuambiana Kifo cha kuambiana chabaini mazito,sumu yatajwa,mke wa ndoa aibuka,uhusiano wake na stara Thomas gumzo.
  3. Kifoc ha Adam Kuambiana kwa Millard Ayo Taarifa za awali kuhusu kifo cha Director Adam Kuambiana.
People.svg Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Adam Kuambiana kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.