Eric Shigongo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Eric James Shigongo (alizaliwa wilayani Buchosa, zamani Sengerema (kabla ya kugawanywa) mkoani Mwanza, 10 Agosti 1969) ni mjasiriamali wa Tanzania ambaye amejikita zaidi katika uandishi wa hadithi na vitabu.

Mpaka sasa ana vitabu vingi kamaː Malkia wa Masokwe, Damu na Machozi, Raisi Anampenda Mke Wangu, Siri Iliyotesa Maisha Yangu, Sheria 10 za Mafanikio na mwisho Maisha ya Mike.

Shigongo ni mwanzilishi na mmiliki wa makampuni ya Global Group ambayo ni: Global Publishers & Ent. Ltd, Global Printways Ltd, Wezesha Mzawa Microfinance Ltd, Dar Live Company Ltd, Shigongo Oil Company Ltd na Blue Mark Real Estate Company Ltd (Kampuni zote hizi zipo Tanzania).

Global Publishers ndiyo inayochapisha magazeti ya Uwazi, Amani, Risasi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi na Spoti Xtra.

Shigongo pia ni mhamasishaji na mwalimu wa masuala ya ujasiriamali, amesaidia vijana wengi kuwafundisha mbinu mbalimbali za kuyatafuta mafanikio kwa kufanya biashara na kujiingizia vipato halali. Miongoni mwa vijana aliowashika mkono ni Ananias Edgar, kijana kutoka Tanzania ambaye ni mtangazaji aliyejikita kwenye simulizi za viongozi mbalimbali Afrika na Duniani, maarufu hasa kutokana na kipaji chake cha kusimulia. Huyo ni zao la Shigongo pia kupitia chombo chake cha habari cha mtandaoni cha Global Tv.

Eric Shigongo ni mtoto wa James Bukumbi na Asteria Kahabi Kapela ambao wote wameshafariki dunia. Mara zote Shigongo amekuwa akisema wazi kwamba wazazi wake walikuwa watu maskini, hakupata bahati ya kusoma sana shuleni lakini alijituma katika biashara zake hadi akafanikiwa.

Siri Iliyotesa Maisha Yangu[hariri | hariri chanzo]

Katika hadithi inayosikitisha ni kitabu cha Siri Inayotesa Maisha Yangu ambayo inamzungumzia mwanadada ambaye aliteseka sana katika maisha yake. Mwanadada huyo aliokotwa na bibi mmoja aliyekuwa na vijana wawili; kwa bahati mbaya bibi huyo alisafiri, basi binti huyo alibakwa na vijana wawili kwa mkupuo.

Tokea hapo binti huyo alitokea kuwachukia wanaume; haikutosha, binti huyo alisaidiwa na mchungaji mmoja ambaye naye lengo kuu ni kumwingilia binti huyo kimwili. Siku moja mchungaji alimwambia binti huyo atengeneze juisi ya matunda, basi binti huyo akatengeneza juisi kama mchungaji alivyosema. Kumbe mchungaji alimwekea madawa ya usingizi kwenye glasi. Baada ya binti huyo kunywa hiyo juisi, mchungaji akamwingilia kimwili. Binti huyo alivyogundua ameingiliwa kimwili na mchungaji huyo, basi tokea hapo hakumwamini mwanamume yeyote, kwani aliamini kila mwanamume ni mdanganyifu na ni mkatili.

Lengo la kitabu ni kwamba tubadilikeː je, wewe ungekuwa mwanadada huyo ungefanya nini?

Inkwell icon - Noun Project 2512.svg Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Eric Shigongo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.