Millard Ayo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Millard Ayo.

Millard Afrael Ayo (amezaliwa Arusha, 26 Januari, 1986) ni mtangazaji, mwandishi wa habari na mwanablogu kutoka nchini Tanzania. Millard anafahamika sana kwa kipindi chake cha Amplifier katika redio Clouds FM. Alianza kutambulika baada ya kujiunga ITV/Radio One mwaka 2008 kabla 2010 kujiunga Clouds FM. Millard Ayo, vilevile anamiliki tovuti ya habari mbalimbali za ndani na nje ya Tanzania inayoitwa millardayo.com ambayo ni moja ya tovuti bora nchini Tanzania. Mbali na hayo, Millard anayo idhaa katika YouTube inaitwa Ayo TV. Idhaa hiyo inatoa habari mbalimbali na inatenda kama TV Mtandaoni.[1]

Ayo amekuwa maarufu Afrika Mashariki kwa uharaka wa kutoa habari kwa muda, matukio kama: siasa, michezo na burudani amekuwa akiyafikisha kwa watu mbalimbali kwa wakati husika.

Tanbihi

  1. Wasifu wa Millard Ayo katika wavuti yake
Inkwell icon - Noun Project 2512.svg Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Millard Ayo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.