Blandina Changula
Blandina Changula | |
---|---|
| |
Jina Kamili | {{{jina kamili}}} |
Jina la kisanii | Johari |
Nchi | Tanzania |
Alizaliwa | 28 Julai 1984 |
Kazi yake | Muigizaji |
Miaka ya kazi | 2001 hadi 2019 |
Ameshirikiana na | Steven Kanumba, Vincent Kigosi,Mwanaidi Suka, Donah Redson nk. |
Kampuni | RJ Company |
Blandina Changula (amezaliwa mkoani Shinyanga, Tanzania, 28 Julai 1984) ni muigizaji wa vipindi vya televisheni na filamu nchini Tanzania.
Maisha ya Mwanzo[hariri | hariri chanzo]
Blandina alipata elimu ya msingi katika shule ya Bugoyi mwaka 1990 hadi 1997 na kujiunga katika shule ya sekondari ya kutwa ya Buluba iliyopo Shinyanga mwaka 1998 hadi 1999.
Akiwa kidato cha pili alihamishiwa katika shule ya bweni ya Kanawa hukohuko mkoani Shinyanga mwaka 1999 hadi 2000 na mwaka huo huo baada ya kuingia kidato cha tatu akahamishiwa tena jijini Dar es Salaam katika shule ya Greens iliyokuwa maeneo ya Temeke kabla ya kuhamishiwa Ubungo shule ambayo alimalizia kidato cha nne hiyo ilikuwa mnamo mwaka 2001.
Blandina Changula anatokea kundi la Kaole Sanaa Group, ni kundi ambalo linafahamika sana nchini Tanzania kwa kutoa nyota wengi waigizaji, Blandina nae ni mmoja kati ya nyota hao, wengine ni Steven Kanumba, Vincent Kigosi (Mr Ray), Thea na wengine wengi tu kutoka Kaole Sanaa Group. Kwa hivi sasa Blandina Chagula kwa kushirikiana na msanii mwenzake Vincent Kigosi wana kampuni yao pamoja iitwayo RJ Company (Ray & Johari company ) ambayo inafanya kazi ya kuzalisha filamu mbalimbali kama vile Bed Rest, Bad Luck , Wrong hope , Peace of mind , Fair Decision nk.
Baadhi ya filamu alizoigiza[hariri | hariri chanzo]
- Sikitiko Langu
- Johari 1 na 2
- Dangerous Desire
- Dar 2 Lagos
Alioshirikiana nao[hariri | hariri chanzo]
- Steven Kanumba
- Vincent Kigosi
- Muhsein Awadh
- Ally Chaowa
- Kulwa Kikumba
- Mwanaidi Suka
- Nuru Nassoro
- Ndumbagwe Misayo
- Donah Redson
- Fatuma Makongoro
- Emmanuel Myamba
- Charles Magari
- Fatuma Mvura
- Mohamed Mwikongi
- Fadhili Omar
Wanigeria[hariri | hariri chanzo]
- Mercy Johnson
- Nkilu Sylvanus
- Nancy Okeke
- Bimbo Ankintola
![]() |
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Blandina Changula kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |