Fatuma Makongoro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Fatuma Makongoro
Amezaliwa
Ikwizu Nyamuswa, Mara
Nchi Tanzania
Kazi yake Mwigizaji


Fatuma Makongoro (maarufu kama Bi Mwenda; alizaliwa kijiji cha Ikwizu Nyamuswa, Wilaya ya Bunda, mkoa wa Mara) ni mtoto wa Mtemi Makongoro, ambaye alikuwa rafiki na ndugu wa yamini na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere [1].

Elimu na maisha yake ya awali[hariri | hariri chanzo]

Bi Mwenda alijiingiza kwenye michezo mbalimbali akiwa darasa la nne. Katika Shule ya Msingi Ikwizu alijihusisha na michezo mbalimbali kama ngoma za asili, netiboli na mbio za kijiti. Alipofika darasa la tano aliamishiwa shule ya Msingi Kinondoni na kwa kipindi chote icho alikuwa akiishi Ikulu.

“Chanzo kinaeleza Bi mwenda alikuwa akijitole, kwa kuwa michezo ilikuwa ndani ya damu”. Bi Mwenda alipomaliza elimu ya msingi, kwa kuwa alikuwa hana kazi nyingine ya kufanya ndipo akaolewa, akiwa ndani ya ndoa alikuwa hajihusishi na jambo lolote zaidi ya kukaa nyumbani kama mama wa familia [2]. Hata hivyo ilipofika mwaka 1998 ndipo alipotamani tena kurudi kwenye michezo hasa na zaidi alivutiwa na uigizaji. Anasema watu ambao kwa kipindi hicho walimvutia sana katika kuigiza alikuwa Mzee Onyango, Mzee Bashir na Mwita Maranya waliokuwa wakiunda kundi la Tausi na wasanii Warid, Richirich, Bishanga ambao walikuwa wakiunda kundi la Mambo Hayo [3].

Kazi yake/Kipaji chake[hariri | hariri chanzo]

Bi Mwenda alianza kazi yake ya sanaa rasmi kupitia kundi liitwalo "Kaole Sanaa Group" katika miaka kumi iliyopita. Kutokana na umahili wake na kipaji alichonacho Bi Mwenda akaweza kudumu kwa miaka mingi katika tasnia hiyo ya filamu.

Filamu/michezo aliyowahi kuigiza[hariri | hariri chanzo]

Mchezo wa kwanza kuigiza na kurushwa uliitwa Kabla Hujafa Hujaumbika ambao Bi Mwenda aliigiza kama mama yake Dk. Cheni. Igizo hilo lilimpatia umaarufu mkubwa, hasa alipoigiza kama mama mchawi, akishirikiana na muigizaji mwenzake mfupi Mlopelo kuwaloga watu na kuwageuza paka.

Chanzo kinaeleza kwenye igizo hilo aliweza kuuva uhusika, ambao ulimpelekea kila mmoja kuwa na mawazo tofauti juu ya uhalisi na uigizaji wake wa uchawi. ilihali hakuwa na lengo lolote zaidi ya kuelimisha jamii kwamba matukio kama hayo yapo. Lakini waandishi na jamii ikaanza kumjadili tofauti,”.

Tangu hapo Bi Mwenda akaanza kupata mialiko ya filamu za nje, wakitaka aigize uhusika wa mama mchawi au mwenye roho mbaya, sababu aliweza kuuvaa uhusika huo vizuri.

Filamu nyingine alizowahi kuigiza na kumpatia umaarufu kutokana na umahiri wake ni kama: Wageni Wangu, Hukumu ya ndoa yangu, Bibi Yangu, Mkono wa Mungu, Binti Mfalme, Kiranga Changu, Subiri Mama, Jungu la Urithi, Witch Doctor, Dendeko, Lupepo Village, Detective, Chozi la Zinaa, Deni la Haki, True Love, Ukungu, From China With Love [4][5]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fatuma Makongoro kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fatuma Makongoro kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.