Kiitalia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Italian language)
Rukia: urambazaji, tafuta

Kiitalia ni lugha inayozungumzwa na watu milioni 70 hasa katika rasi ya Italia.

Ni lugha rasmi ya Italia, San Marino, Vatikano, Uswisi na katika sehemu za Slovenia na Kroatia.

Inatumika pia katika Monako, Malta, Albania na visiwa kadhaa za Ugiriki), halafu bado kama lugha ya elimu katika nchi zilizokuwa makoloni ya Italia kama Eritrea, Libya, Ethiopia na Somalia.

Kihistoria asili yake ni lugha ya Kilatini, hivyo pamoja na Kifaransa, Kihispania, Kireno, Kiromania na lugha nyingine ndogo ni moja ya lugha za Kirumi.

Blau: Amtssprache; Hellblau: Verkehrssprache ItalophoneEuropeMap.png
Kiitalia

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]