Flaviano wa Kostantinopoli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Flaviano wa Konstantinopoli)
Mt. Flaviano.

Flaviano wa Konstantinopoli (kwa Kigiriki Φλαβιανος, Phlabianos; kwa Kilatini Flavianus; alifariki Hypaepa, Lydia, leo Uturuki, 11 Agosti 449), alikuwa Patriarki wa Konstantinopoli tangu 446 hadi 449.

Anaheshimiwa tangu kale na Wakatoliki na Waorthodoksi[1] kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 16 Februari, 17 Februari[2] na pia 24 Novemba.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Flaviano alikuwa mlinzi wa vyombo vitakatifu vya Kanisa la Konstantinopoli. Kutokana na sifa yake ya utakatifu alichaguliwa kuwa askofu mkuu wa jiji hilo.

Alipowekwa wakfu na kutawazwa, kaisari Theodosius II alikuwa Kalsedonia. Towashi wake Khrisafyo alijaribu kumdai Flaviano zawadi ya dhahabu kwa ajili ya kaisari, lakini alipokataliwa alifanya njama dhidi yake kwa kumuunga mkono Eutike, mpinzani wa Flaviano.

Flaviano aliongoza mtaguso wa maaskofu 40 huko Konstantinopoli tarehe 8 Novemba 448 ili kumaliza mgogoro kati ya askofu mkuu wa Sardi na maaskofu wawili wa kanda yake. Hapo askofu Eusebius wa Dorylaeum alileta shtaka dhidi ya Eutike. Flaviano alitaka apewa muda wa kuonywa, lakini sinodi ilimuondoa Eutike.

Kwa kuwa huyo alilalamika na kupata sapoti ya Dioskoro I wa Aleksandria, kaisari aliitisha mtaguso mwingine huko Efeso. Huko tarehe 8 Agosti 449, Eutike na Dioskoro walimshambulia vikali Flaviano ambaye siku tatu baadaye alifariki dunia kutokana na mapigo aliyoyapata.[3]

Matokeo[hariri | hariri chanzo]

Papa Leo I, ambaye wajumbe wake walipuuziwa katika huo mtaguso, alilalamika kwa kuuita "sinodi ya wizi" akafuta maamuzi uliyoyatoa.

Baada ya Theodosius II kufa mwaka 450, dada yake Pulkeria alirudi madarakani, akioana na afisa Marchano, ambaye akawa kaisari. Hao wawili walirudisha masalia ya Flaviano Konstantinopoli kwa namna ya "maandamano ya ushindi ... si mazishi".

Mtaguso wa Kalsedonia (451) alilaani mafundisho ya Eutike, alithibitisha "Hati kwa Flaviano" ya Papa Leo (barua 28[4] na kumtangaza Flaviano kuwa mfiadini.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Menaion, read in Συναξάριον
  2. Martyrologium Romanum
  3. Among the documents which touch on the career of Flavian are the reply of Petrus Chrysologus, archbishop of Ravenna, to a circular appeal of Eutyches, and various letters of Theodoret. Pope Leo I wrote Flavian a beautiful letter before hearing that he was dead.
  4. Pope Leo I. Letter 28 - The Tome. New Advent. Iliwekwa mnamo 2011-02-18.

Vyanzo[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.