Busia, Uganda
Busia | |
Mahali pa mji wa Busia katika Uganda |
|
Majiranukta: 00°28′01″N 34°05′20″E / 0.46694°N 34.08889°E | |
Nchi | Uganda |
---|---|
Mkoa | Mashariki |
Wilaya | Busia |
Serikali | |
- Mayor | Michael Mungeni |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 43,200 |
Busia ni mji katika mashariki mwa Uganda. Huu ndio mji mkubwa katika Wilaya ya Busia na makao makuu ya wilaya yako hapo.
Mahali
[hariri | hariri chanzo]Busia iko kwenye mpaka na Kenya. Mji huu ni takriban kilometre 202 (mi 126) kwa barabara, mashariki kwa Kampala, jiji kubwa na mji mkuu wa Uganda. [1]
Idadi ya Watu
[hariri | hariri chanzo]Katika mwaka 2002, sensa ya kitaifa ilihesabu idadi ya wakazi Busia, Uganda, kuwa 36,630. Mwaka 2008, Uganda Bureau of Statistics ilikadiria idadi ya wakazi wa mji huu kuwa 43,200. [2]
Shughuli za Kiuchumi
[hariri | hariri chanzo]Mji huu, pamoja na mji dada yake wa Busia, Kenya kando ya mpaka, ni vituo vya shughuli za biashara kubwa na trafiki ni nzito katika pande zote mbili. Bidhaa kutoka Uganda ni pamoja na mazao ya biashara kama kahawa, pamba na mbao zinazopelekwa katika bandari ya Mombasa nchini Kenya kwa ajili ya kuuza nje. Vyakula kama ndizi, mananasi na maembe zinazopelekwa kwa soko ya Kenya pia hupita mpakani. Kwa upande mwingine, Uganda huagiza mafuta ya petroli, bidhaa za viwandani na nyumbani kama mafuta ya kupikia, sabuni, nguo,vifaa vya elektronik na magari.
Busia ndio mji wa shughuli nyingi sana mpakani kati ya nchi hizi mbili jirani wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mji wa mpaka wa Malaba ulioko takribani kilometre 46 (mi 29) kaskazini, ni wa pili kwa shughuli za biashara kati ya Uganda na Kenya katika eneo la pamoja la mpaka wao. Tazama jadwali hapa chini:
Kiwango cha biashara kwa miji iliyoko kwenye mpaka za Uganda mwaka 2005 | |||
Nambari | Mji ulioko mpakani | Kiwango cha mauzo ya kutoka | Kiwango cha mauzo ya kuingia |
---|---|---|---|
1 | Busia | 42.7% | 54.3% |
2 | Mpondwe | 25.0% | 10.6% |
3 | Malaba | 7.8% | 19.9% |
4 | Paidha | 9.3% | 2.2% |
5 | Mingine | 15.2% | 13.0% |
Jumla | 100.0% | 100.0% |
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Angalia Pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Uganda bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Busia, Uganda kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |