Bad
Bad | |||||
---|---|---|---|---|---|
Studio album ya Michael Jackson | |||||
Imetolewa | 31 Agosti 1987 | ||||
Imerekodiwa | Novemba 1986–Julai 1987 (kasoro Another Part of Me: ilirekodiwa 1985) | ||||
Aina | Soul, R&B, Dansi-pop, Urban, Pop rock[1] | ||||
Urefu | 48:16 | ||||
Lebo | Epic EK-40600 |
||||
Mtayarishaji | Michael Jackson, Quincy Jones[2] |
||||
Tahakiki za kitaalamu | |||||
|
|||||
Wendo wa albamu za Michael Jackson | |||||
|
|||||
Single za kutoka katika albamu ya Bad | |||||
|
Bad ni jina la kutaja albamu ya saba ya mwanamuziki, mtayarishaji wa rekodi, mwimbaji, mfanyabiashara, kabaila, na mhisani wa Kimarekani, Michael Jackson. Albamu ilitolewa mnamo tar. 31 Agosti 1987 na studio ya Epic/CBS Records. Rekodi ya albamu hii ilitolewa karibuni miaka mitano tangu kutoka kwa albamu ya awali. Miaka ishirini baada ya kutolewa, albamu imeuza takriban nakala zaidi ya milioni 30 kwa dunia nzima, na kopi milioni 8 ziliuzwa nchi za nje kwa kupitia Marekani peke yake. Bad ni albamu ya kwanza, na ndiyo hadi sasa albamu pekee, iliyoweza kuingiza single tano katika Billboard Hot 100 zikiwa nafasi ya 1.[3]
Katika albamu hii, Jackson ameonekana kuwa huru zaidi kupita zile albamu zake za mbili za awali, Off the Wall na albamu yenye mauzo bora kwa muda wote, Thriller. Humu katunga nyimbo tisa katika kumi na moja za albamu, na amesaidia kutunga na kutayarisha wimbo wa "Man in the Mirror". Pia humu amekuja na sura mpya ya mshangao.
Albamu iliendelea kupata mafanikio makubwa katika miaka ya 1980 na imeshinda tuzo mbili za Grammy, moja kwa Muziki Bora wa Video - Leave Me Alone na nyingine kwa ajili ya Uhandisi Bora wa Albamu, Bruce Swedien na Humberto Gatica.[4] Mnamo mwaka 2009, Bad pia, imewekwa nafasi ya 43 katika orodha ya Albamu Bora 100 za Karne za MTV zilizoorodheshwa na VH1.[5] Albamu pia iliwekwa nafasi ya 202 katika orodha ya gazeti ya Rolling Stone, Albamu Bora ya Karne.[6]
Historia
[hariri | hariri chanzo]Orodha ya nyimbo
[hariri | hariri chanzo]# | Jina | Mtunzi (wa) | Urefu |
---|---|---|---|
1. | "Bad" | Michael Jackson | 4:07 |
2. | "The Way You Make Me Feel" | Jackson | 4:58 |
3. | "Speed Demon" | Jackson | 4:03 |
4. | "Liberian Girl" | Jackson | 3:53 |
5. | "Just Good Friends" (kaimba na Stevie Wonder) | Terry Britten, Graham Lyle | 4:08 |
6. | "Another Part of Me" | Jackson | 3:54 |
7. | "Man in the Mirror" | Glen Ballard, Siedah Garrett | 5:19 |
8. | "I Just Can't Stop Loving You" (kaimba na Siedah Garrett) | Jackson | 4:13 |
9. | "Dirty Diana" | Jackson | 4:40 |
10. | "Smooth Criminal" | Jackson | 4:17 |
Toleo la CD la 1988 | |||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
# | Jina | Mtunzi (wa) | Urefu | ||||||
11. | "Leave Me Alone" | Jackson | 4:38 |
"Toleo Maalumu" la 2001 [7] | |||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
# | Jina | Mtunzi (wa) | Urefu | ||||||
12. | "Interview with Quincy Jones #1" | 4:03 | |||||||
13. | "Streetwalker" (Awali haikutolewa) | Jackson | 5:49 | ||||||
14. | "Interview with Quincy Jones #2" | 2:53 | |||||||
15. | "Todo Mi Amor Eres Tu" (Toleo la Kihispania la "I Just Can't Stop Loving You", awali haikupatikana) | Jackson, Rubén Blades | 4:05 | ||||||
16. | "Interview with Quincy Jones #3" | 2:30 | |||||||
17. | "Spoken intro to Fly Away" | 0:08 | |||||||
18. | "Fly Away" (Awali haikutolewa) | Jackson | 3:26 |
Toleo la pili la Bad limekuwa na utofauti fulani ukifananisha na lile toleo la mwaka wa 1987:[8]
- "Bad" inabadiliko ya utayarishaji.
- "The Way You Make Me Feel" ina utajiri wa sauti za nyuma kuliko ya awali.
- "I Just Can't Stop Loving You" imeondosha maneno ya mwanzo ya Jackson.
- "Dirty Diana" imeongezeka kidogo.
- "Smooth Criminal" imeondosha pumzi za kigiizaji na intro.
Single zake
[hariri | hariri chanzo]- Julai 1987 - "I Just Can't Stop Loving You" U.S. #1 / UK #1
- Septemba 1987 - "Bad" U.S. #1 / UK #3
- Novemba 1987 - "The Way You Make Me Feel" U.S. #1 / UK #3
- Januari 1988 - "Man in the Mirror" U.S. #1 / UK #21
- Aprili 1988 - "Dirty Diana" U.S. #1 / UK #4
- Julai 1988 - "Another Part of Me" U.S. #11 / UK #15
- Septemba 1988 - "Smooth Criminal" U.S. #7 / UK #8
- Januari 1989 - "Leave Me Alone" UK #2
- Juni 1989 - "Liberian Girl" UK #13[9]
Chati zake
[hariri | hariri chanzo]Chati (1987) | Nafasi iliyoshika |
---|---|
Australia | 2 |
Austria | 1 |
Brazil | 1 |
Kanada | 1 |
Ufaransa | 1 |
Ujerumani | 1 |
Italia | 1 |
Japani | 1 |
Uholanzi | 1 |
New Zealand | 1 |
Norwei | 1 |
Sweden | 1 |
Switzerland | 1 |
UK Albums Chart | 1 |
U.S. Billboard 200 | 1 |
U.S. R&B/Hip-Hop Albums | 1 |
Matunukio
[hariri | hariri chanzo]Nchi | Matunikio | Nchi za nje |
---|---|---|
Australia | 5x Platinamu | 350,000 |
Austria | 4x Platinamu | 80,000 [10] |
Brazil | Diamond | 1,100,000 |
Kanada | 7x Platinamu | 700,000 |
Ufaransa | Almasi | 1,400,000 |
Ujerumani | 4x Platinamu | 2,000,000 |
Japani | Almasi | 1,000,000 |
Hispania | 7x Platinamu | 500,000 |
UK | 13x Platinamu | 3,600,000 |
U.S. | 8x Platinamu | 8,100,000 |
Mauzo ya Marekani
[hariri | hariri chanzo]Kipindi | Tuzo ya RIAA | Kupeleka nchi za nje kutoka U.S. | Jumla |
---|---|---|---|
Aug 31, 1987 - Nov 9, 1987 | Gold, Platinum na 3x Platinum mnamo Nov 9, 1987 | 3,000,000 | 3,000,000 |
Nov 10, 1987 - Dec 31, 1987 | 4x Platinum mnamo Dec 31, 1987 | 1,000,000 | 4,000,000 |
Jan 1, 1988 - Mar 21, 1988 | 5x Platinum mnamo Mar 21, 1988 | 1,000,000 | 5,000,000 |
Mar 22, 1988 - Jun 1, 1988 | 6x Platinum mnamo Jun 1, 1988 | 1,000,000 | 6,000,000 |
Jun 2, 1988 - Aug 25, 1993 | 7x Platinum mnamo Aug 25, 1993 | 1,000,000 | 7,000,000 |
Aug 26, 1993 - Sep 29, 1994 | 8x Platinum mnamo Sep 29, 1994 | 1,000,000 | 8,000,000 |
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Bad". AllMusic. Iliwekwa mnamo 2009-04-27.
- ↑ "Album Credits for Bad". Artists Direct. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-07-14. Iliwekwa mnamo 3 Februari 2006.
{{cite web}}
: Unknown parameter|dateformat=
ignored (help) - ↑ "MTV - Michael Jackson Biography". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-06-17. Iliwekwa mnamo 2009-07-03.
- ↑ "Grammy for Bruce Swedien & Humberto Gatica". Grammy. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-06-20. Iliwekwa mnamo 2009-02-25.
- ↑ Bowman, Edith. "VH1 - Greatest Albums Ever". VH1. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-03-10. Iliwekwa mnamo 9 Aprili 2009.
- ↑ "The RS 500 Greatest Albums of All Time". Rolling Stone. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-06-23. Iliwekwa mnamo 18 Novemba 2003.
- ↑ "Bad/Dangerous". www.amazon.co.uk. Iliwekwa mnamo 2008-08-25.
- ↑ Michael Jackson: Kwa upande wa rekodi. Chris Cadman, Michael Haystead.
- ↑ Michael Jackson , The Ultimate Collection, Booklet
- ↑ IFPI Austria - Verband der Österreichischen Musikwirtschaft
Maelezo
[hariri | hariri chanzo]- Taraborrelli, J. Randy (2004). The Magic and the Madness. Terra Alta, WV: Headline. ISBN 0-330-42005-4.