Kitabu cha Malaki
Kitabu cha Malaki ni cha mwisho kati ya vitabu 12 vya Manabii wadogo ambavyo, pamoja na vingine vingi, vinaunda Tanakh, yaani Biblia ya Kiebrania. Hivyo ni pia sehemu ya Agano la Kale katika Biblia ya Kikristo, na kwa kuwa humo vitabu vya manabii vinapangwa baada ya vitabu vya hekima, kitabu cha Malaki ni cha mwisho kabla ya vitabu vya Agano Jipya.
Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.
Mwandishi na jina
[hariri | hariri chanzo]Kwa kuwa jina la nabii aliye asili ya kitabu hiki halijulikani, limetumika lile la neno lake muhimu zaidi, "Malaki", lenye maana ya "Mjumbe wangu" (kwa Kiebrania מלאכי).
Muda
[hariri | hariri chanzo]Yaliyomo yanawezesha kukisia kiliandikwa lini, yaani baada ya Hekalu la Yerusalemu kuwekwa wakfu (515 K.K.), na kabla ya katazo la ndoa za mseto kati ya Wayahudi na mataifa mengine lililotolewa na Nehemia (445 K.K.); sanasana ni karibu na mwaka huo.
Muhtasari
[hariri | hariri chanzo]Kitabu kinaundwa na sehemu sita za namna ileile: Mungu (au nabii wake) anatoa kauli ambayo inajadiliwa na waamini na makuhani wao, halafu inafafanuliwa katika hotuba inayochanganya vitisho na ahadi za wokovu.
Mada kuu ni mbili: makosa ya makuhani na waamini wengine katika ibada, halafu makwazo yanayosababishwa na ndoa za mseto.
Nabii anatabiri siku ya YHWH atakayetakasa makuhani, ataangamiza waovu na kuwapa ushindi waadilifu.
Mistari ya mwisho, ikitabiri ujio wa pili wa nabii Eliya, ilivutia sana tumaini la Wayahudi; ndiyo sababu ilijadiliwa sana kuhusiana na Yohane Mbatizaji na Yesu Kristo, kama inavyoonekana katika sehemu mbalimbali za Injili.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- New American Bible - http://www.usccb.org/nab/bible/malachi/malachi1.htm Ilihifadhiwa 28 Julai 2011 kwenye Wayback Machine.
- 21st Century KJV - http://www.biblegateway.com/passage/?search=Malachi+1&version=KJ21
- NIRV - http://www.biblegateway.com/passage/?search=Malachi+1&version=NIRV
- Malachi at Chabad.org - http://www.chabad.org/library/bible_cdo/aid/16219
- Easton's Bible Dictionary, 1897.
- Hill, Andrew E. Malachi: A New Translation with Introduction and Commentary. The Anchor Bible Volume 25D. Toronto: Doubleday, 1998.
- LaSor, William Sanford et al. Old Testament Survey: the Message, Form, and Background of the Old Testament. Grand Rapids: William B. Eerdmans, 1996.
- Mason, Rex. The Books of Haggai, Zechariah and Malachi. The Cambridge Bible Commentary on the New English Bible. New York, Cambridge University Press, 1977.
- Singer, Isidore & Adolf Guttmacher. "Book of Malachi." JewishEncyclopedia.com. 2002.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Van Hoonacker, A. "Malachias (Malachi)." Catholic Encyclopedia. Transcribed by Thomas J. Bress. 2003.
- The Oracle of Malachi Ilihifadhiwa 4 Aprili 2013 kwenye Wayback Machine. - A verse-by-verse journey through Malachi, connecting 2,500 years ago with today.
Mwanzo * Kutoka * Walawi * Hesabu * Kumbukumbu * Yoshua * Waamuzi * Ruthu * Samueli I * Samueli II * Wafalme I * Wafalme II * Mambo ya Nyakati I * Mambo ya Nyakati II * Ezra * Nehemia * TobitiDK * YudithiDK * Esta * Wamakabayo IDK * Wamakabayo IIDK * Yobu * Zaburi * Methali * Mhubiri * Hekima DK * SiraDK * Wimbo Bora * Isaya * Yeremia * Maombolezo * BarukuDK * Ezekieli * Danieli * Hosea * Yoeli * Amosi * Obadia * Yona * Mika * Nahumu * Habakuki * Sefania * Hagai * Zekaria * Malaki
Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kitabu cha Malaki kama historia yake au athari wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |