YHWH
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
YHWH kwa alfabeti ya Kiebrania cha zamani (karne ya 10 KK hadi 135 BK), ya Kiaramu cha zamani (karne ya 10 KK hadi karne ya 4 BK) na ya mraba (karne ya 3 hadi sasa).
Ukuta wa mbele wa Basilika ya Mt. Louis, lililojengwa mwaka 1834 huko St. Louis, Missouri, una jina hilo upande wa juu.
Herufi nne יהוה (YHWH) ni konsonanti za jina la Mungu linalopatikana mara 6,828 katika Biblia ya Kiebrania kuanzia Mwa 2:4. Halipatikani katika vitabu vya Wimbo Ulio Bora, Kitabu cha Mhubiri na Kitabu cha Esta.
[hariri] Matamshi
Matamshi sahihi ya jina hilo hayajulikani kwa hakika, lakini leo wengi wanalitamka Yahweh.