Winnie Mandela

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Winnie Madikizela-Mandela
Winnie Mandela00.jpg
Amezaliwa 26 Septemba 1936 (1936-09-26) (umri 81)
Bizana, Afrika Kusini
Nchi South African
Mshahara US$ 100,000
Ndoa Nelson Mandela
Watoto Zenani Mandela,
Zindzi Mandela-Hlongwane
Tovuti www.anc.org.za

Winnie Madikizela-Mandela (amezaliwa tar. 26 Septemba 1936 na jina la Nomzamo Winifred Zanyiwe Madikizela ) ni mwanasiasa wa Afrika Kusini, ambaye ameshikilia nafasi kadhaa serikalini na alikuwa mkuu wa ligi ya wanawake African National Congress (ANC). Wakati huu yeye ni mwanachama wa kamati ya kimataifa ya ANC. Ingawa bado alikuwa mke wa Nelson Mandela wakati Mandela alipewa urais wa Afrika ya Kusini mnamo Mei 1994, kamwe hakuwa mwanamke wa kwanza wa Afrika ya Kusini, kwani wanandoa hawa walikuwa wametengana miaka miwili iliyopita. Hii ilikuwa baada ya Winnie kugunduliwa kuwa na uhusiano wa kimapemzi na watu wengine baada ya kuachiliwa kwa Nelson kutoka gerezani mnamo Februari 1990. Talaka ya mwisho ilipitishwa mnamo tarehe 19 Machi 1996.

Kama mwanaharakati mwenye utata, yeye ni maarufu miongoni mwa wafuasi wake ambao humwita 'Mama wa Taifa'.Lakini si wote wanaompenda kwani wengine humtusi, hasa kutokana na madai kadhaa ya uhusika wake katika ukiukaji wa haki za binadamu, iliyohusisha mateso na mauaji ya mtoto wa umri wa miaka 14 aliyekuwa anaitwa Stompie Moeketsi mwaka wa 1989.

Mnamo Machi 2009, tume huru ya Uchaguzi ilitawaza kwamba Winnie Mandela, ambaye alikuwa amechaguliwa kama mgombea wa ANC, anaweza kukimbia kiti katika uchaguzi mkuu mwa Aprili 2009, licha udanganyifu kushtakiwa.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Miaka ya awali[hariri | hariri chanzo]

Jina lake la kixhosa ni Nomzamo . Nomzamo yamaanisha "yule ambaye anajaribu". Alizaliwa katika kijiji cha Mbongweni [5] Bizana, katika mkoa wa Pondo ambayo sasa ni mkoa wa Eastern Cape huko Afrika Kusini. Alikuwa amefanya idadi ya ajira katika maeneo mbalimbali ambayo wakati huo yalikuwa yanajulikana kama Banstustan ya Transkei, pamoja na serikali ya Transkei. Nyakati mbalimbali alikuwa akiishi katika sehemu za Bizana, Shawbury, na Johannesburg.

Alikutana na mwanasheria na mwanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi, Nelson Mandela, mwaka wa 1957. Walifunga ndoa mwaka wa 1958 na kujaliwa kupata binti wawili, Zenani (aliyezaliwa mwaka wa 1959) na Zindzi (aliyezaliwa mwaka wa1960). Winnie ana ugonjwa wa sukari.

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Licha ya vikwazo vya elimu kwa Waafrika wakati wa ubaguzi wa rangi, alichuma shahada katika kazi za kijamii kutoka Shule Jan Hofmeyer huko Johannesburg, na miaka kadhaa baadaye alichuma shahada katika kozi ya mahusiano ya kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Witwatersrand, ambacho pia kiko Johannesburg.

Ubaguzi wa Rangi[hariri | hariri chanzo]

Alijitokeza kama kiongozi mpinzani wa utawala kwa wazungu wachache serikalini wakati mumewe aliwekwa jela kwa muda mrefu (kuanzia Agosti 1963 hadi Februari 1990). Kwa miaka mingi, alipelekwa katika mji wa Brandfort katika eneo la Orange Free State na kuchungwa katika sehemu hiyo, isipokuwa nyakati alizoruhusiwa kumtembelea mumewe jelani katika kisiwa cha Robben.

Katika miaka ya 1980 na mapema 1990, alivutia kwa ukubwa makini ya vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa na kumpelekea kuhojiwa na wanahabari wengi wa kigeni na vilevile wanahabari wa kitaifa kama Jani Allan, ambaye wakati huo alikuwa mwanandishi katika gazeti lililokuwa linaongoza la Sunday Times

Katika barua moja kwa Jacob Zuma mnamo Oktoba 2008, rais aliyejiuzulu wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki, alionyesha jukumu lililoumbwa na ANC kwa ajili ya Winnie katika harakati za kupambana na ubaguzi wa rangi:

Katika muktadha wa mapambano ya kimataifa kwa ajili ya kutolewa kwa wafungwa wa kisiasa katika nchi yetu, harakati yetu ilichukua uamuzi wa kimakusudi kumweka Nelson Mandela kama mwakilishi wa wafungwa hawa, na hivyo kutumia wasifu wake wa kibinafsi wa kisiasa, pamoja na mateso ya mkewe wa awali, Winnie Mandela, kuonyesha dunia na jamii ya Afrika Kusini ukatili wa mfumo wa ubaguzi wa rangi.

Lugha ya vurugu na madai ya mauaji[hariri | hariri chanzo]

Sifa yake iliharibika kutokana na maneno aliyozungumza. Watu wengi walifikiria lugha aliyotumia ilichangamsha damu ya watu wakati mwingine. Mfano mzuri ni wakati alitoa hotuba katika eneo la Munsieville tarehe 13 Aprili 1985, ambapo alifanya mazoezi ya necklacing (kuwachoma watu hai kutumia gurudumu na petroli) katika mapambano kukomesha ubaguzi wa rangi. Alisema, "pamoja na masanduku yetu ya viberiti na mashanga yetu tutaokoa nchi hii".

Sifa yake iliharibiwa zaidi na shutuma za askari wake, Jerry Richardson. Jerry alisema Winnie Madikizela-Mandela aliamrisha utekaji nyara na uuaji Tarehe 29 Desemba 1989, Richardson alimteka nyara James Seipei (pia alikuwa anajulikana kama Stompie Moeketsi) aliyekuwa na umri wa miaka 14 na vijana wengine watatu kutoka katika nyumba ya Mchungaji Paul Verryn. Bi. Mandela alidai kuwa aliamrisha vijana hawa kupelekwa nyumbani kwake kwa sababu alidhani vijana hawa walikukuwa wanatumiwa kwa ngono. Wanne hao walipigwa ili wakubali kuwa walifanya ngono na Seipei alishtakiwa kuwa msiri. Mwili wa Seipei ulipatikana katika uwanja majeraha ya kudungwa kooni tarehe 6 Januari 1990. Tukio hili likawa sababu ya serikali ya kibaguzi kujulikana. Mwaka 1991, alipatikana na hatia ya utekaji nyara na kuwa mhusika katika kifo cha Seipei. Kisha alifungwa jela lakini miaka yake jelani ilipunguzwa kwa rufaa ya faini.

Baada ya Ubaguzi wa rangi[hariri | hariri chanzo]

Wakati Afrika Kusini ilikuwa ina badilika kuwa demokrasia ya mpito, tabia yake kwa wazungu haikuwa kama ya mumewe. Ingawa alikuwa kando ya mumewe alipoachiliwa mwaka wa 1990, wakati wa kwanza hao wawili walionekana na umma kwa karibu miaka thelathini, ndoa ya Mandela ya miaka 38 ilimalizika walipotengana mnamo Aprili 1992 baada ya kujulikana kwamba yeye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na watu wengine wakati Nelson alikuwa amefungwa. Winnie alipewa talaka mnamo Machi 1996. Kisha alianza kutumia jina Madikizela-Mandela. Alipewa cheo cha naibu wa Waziri wa Sanaa, Utamaduni, Sayansi na Teknolojia katika serikali ya kwanza baada ya ubanguzi wa rangi (Mei 1994). Alifutwa kazi baada ya miezi 11 kufuatia madai ya rushwa.

Alibakia maarufu miongoni mwa wafuasi wengi wa ANC, na, mnamo Desemba 1993 na Aprili 1997, yeye aliteuliwa rais wa ligi ya wanawake ya ANC, ingawa alitoa ugombeaji wake wa Naibu wa Rais wa ANC katika mkutano wa harakati hiyo mnamo Desemba 1997.

Mwaka 1997, aliitokeza mbele ya tume ya Ukweli na Maridhiano (Truth and Reconciliation Commission). Mwenyekiti wa tume hii alikuwa Askofu Mkuu Desmond Tutu na alitambua umuhimu wake katika harakati za kupambana na ubaguzi wa rangi, lakini pia alimwomba aombe msamaha na kukubali makosa yake. Katika majibu yake, alirudia maneno ya Askofu Mkuu na kukubali kwamba mambo yalienda mrama.

Mashtaka ya Udanganyifu na Wizi[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 24 Aprili 2003, alipatikana na hatia ya makosa 43 ya udanganyifu na 25 ya wizi, na ajenti wake, Addy Moolman, alipatikana na hatia ya makosa 58 ya udanganyifu na 25 ya wizi. Wote wawili walikuwa wamekana mashtaka hayo, ambayo yalihusisha fedha zilizochukuliwa kutoka akaunti ya mkopo ya wanachama ya mazishi, lakini wanachama hawakufaidika. Madikizela-Mandela alihukumiwa miaka mitano jelani.

Muda mfupi baada ya kushtakiwa, alijiuzulu kutoka nafasi zote za uongozi za ANC, pamoja na kiti chake cha ubunge na urais wa ligi ya wanwake ya ANC.

Mwishoni mwa mwaka 2003, rafiki wake wa dhati Hazel Crane aliuawa. Awali Crane aljitoa kununua nyumba ya Madikizela-Mandela.

Mnamo Julai 2004, jaji wa rufaa wa Mahakama Kuu ya Pretoria alitawaza kwamba " uhalifu haukufanyika kwa faida za kibinafsi". Hakimu alipindua shtaka la wizi, lakini shtaka la udanganyifu lilibaki, kisha akahukumiwa miaka 3 na miezi 6.

Kunyimwa visa na Kanada[hariri | hariri chanzo]

Mnamo Juni 2007, Balozi wa Kanada nchini Afrika Kusini lilikata kumruzuku Winnie Mandela visa ya kusafiri kwenda Toronto, Kanada, ambapo alikuwa amepangiwa kuhudhuria sherehe ya kuchanga pesa iliyoandaliwa na shirika la sanaa la MusicaNoir, ambayo ilikuwa pamoja na siku ya kwanza ya kuonyeshwa kwa The Passion ya Winnie , opera kumhusu Winnie.

Kurudi kwenye siasa[hariri | hariri chanzo]

Wakati ANC ilitangaza Uchaguzi wa Kamati yake ya Utendaji wa Kitaifa mnamo tarehe 21 Desemba 2007, Mandela alikuwa wa kwanza na kura 2845.

Kuomba msamaha kwa Walioathirika[hariri | hariri chanzo]

Mandela alishtumu ghasia za upambanaji wa wahamiaji kuanzia Mei hadi Juni 2008 ambayo ilianza Johannesburg na kuenea nchini kote, na alililaumu serikali kukosa makazi yafaayo kutokana na hisia za maandamano. Pia aliomba msamaha walioathirika kutokana na maandamano [29] na alitembelea mji Alexandra.

Pia alijitolea kutumia nyumba yake kama malazi kwa familia ilyoingia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. ] Alionya kuwa wahusika wa ghasia wangegoma kwenye mfumo wa gari la moshi la Gauteng. [

Uchaguzi mkuu 2009[hariri | hariri chanzo]

Mandela alipata nafasi ya tano katika orodha ya uchaguzi ya ANC katika uchaguzi mkuu wa 2009, nyuma ya rais wa chama na Rais wa sasa wa Afrika ya Kusini Jacob Zuma, Rais wa kitambo wa South Africa Kgalema Motlanthe, Naibu wa Rais wa South Afrika Baleka Mbete, na Waziri wa Fedha Trevor Manuel. Makala katika gazeti la The Observer ilipendekeza kwamba msimamo wake juu ya orodha ilionyesha kuwa uongozi wa chama uliona thamani yake kama mali muhimu katika uchaguzi kuhusu kuongeza ufuasi kati ya mashinani ya chama na maskini .

Kuonyeshwa kwake katika Filamu na Runinga[hariri | hariri chanzo]

Tina Lifford anacheza kama Mandela katika kipindi cha runinga cha mwaka wa 1997, Mandela and De Klerk . Sophie Okonedo anacheza kama Mandela katika kipindi cha televisheni ya BBC ya Mrs. Mandela , inayotarajiwa kuonyeshwa mwaka wa 2009. Jennifer Hudson atacheza kama Winnie katika filamu itakayoanza kutengenezwa mnamo Mei 2010.

Jennifer Hudson amepewa fursa ya kucheza kama Winnie Mandela katika filamu hiyo inayojulikana kama "Winnie", itakayoongozwa na Darrell J. Roodt Andre Pieterse, Roodt na Paulo L. Johnson alitunga filamu hii kutokana na wasifu wa Winnie Mandela (“"Winnie Mandela: A Life" [37]”) ilyoandikwa na Anne Marie du Preez Bezdrob. Umoja wa Wafanyikazi wa Creative wa Afrika Kusini umepinga uchaguzi huu, na kusema itachelewesha kutengenezwa kwa filamu hii iwapo wahusika hawatabadilishwa.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]