Nenda kwa yaliyomo

Rasi ya Mashariki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Eastern Cape)
Jimbo la Rasi ya Mashariki
Eastern Cape Province
Oos-Kaap
Mpuma-Koloni
(Nembo la Rasi Mashariki)
Mahali pa Rasi Mashariki
Mji Mkuu Bisho
Mji Mkubwa Port Elizabeth
Waziri Mkuu Phumulo Masualle
Eneo
Nafasi kati ya majimbo
- Jumla

ya 2

169,580 km²
Wakazi
Nafasi kati ya majimbo
 - Jumla (2001)
 - Msongamano wa watu

ya 3

6,436,761
38/km²
Lugha Kixhosa (83%)
Kiafrikaans (9.6%) Kiingereza (3.7%)
Wakazi kimbari Waafrika Weusi (87.6%)
Chotara (7.4%)
Wazungu (4.7%)
Asili ya Asia (0.3%)
edit


Rasi ya Mashariki ni kati ya majimbo 9 za Afrika Kusini. Iliundwa mwaka 1994 baada ya mwisho wa siasa ya Apartheid. Mji mkuu ni Bisho. Jimbo lilianzishwa 1994 wakati wa mwisho wa siasa ya Apartheid kwa kuungaisha sehemu ya mashariki ya Jimbo la Rasi la awali na bantustan za Ciskei na Transkei.

Wakazi na utamaduni

[hariri | hariri chanzo]

Jumla ya wakazi ni milioni sita na nusu. Walio wengi ni Waxhosa na Kixhosa ni lugha ya kwanza jimboni. Lugha ya pili ni Kiafrikaans hasa katika kusini.

Miji muhimu pamoja na Bisho ni Port Elizabeth, East London, Grahamstown, King William's Town, Queenstown, Uitenhage, Mthatha, Aliwal North na Cradock.

Rasi Mashariki ni jimbo maskini zaidi nchini. Sababu yake ni hasa umaskini kali katika bantustan za zamani yaani maeneo ya Ciskei na Transkei ambako watu wengi ni wakulima wadogo-wadogo wanaolima mashamba madogo mno.

Miji miwili kuna ajira ya viwandani ni Port Elizabeth na East London. Viwanda vya motokaa vya General Motors, Volkswagen na DaimlerChrysler ni uti wa mgongo wa uchumi wa eneo.

Kaskazini ya Port Elizabeth kunatokea ujenzi wa bandari mpya kwa Coega.

Watu wa Rasi Mashariki

[hariri | hariri chanzo]

Maraisi wa taifa Nelson Mandela na Thabo Mbeki wote ni wenyeji wa jimbo.

Marejeo ya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Rasi ya Mashariki kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.