Nenda kwa yaliyomo

Uchaguzi nchini Kenya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Uchaguzi Nchini Kenya)
Jamhuri ya Kenya

Makala hii imepangwa kwa mfululizo:
Siasa na serikali ya
Kenya



Nchi zingine · Atlasi


Uchaguzi Mkuu nchini Kenya hufanyika baada ya kila miaka mitano. Katika miaka ya hivi karibuni. Kenya imekuwa ikikumbwa na mizozo wakati wa uchaguzi, kwa mfano shuhudio la uchaguzi wa urais mnamo 2007. Ingawa mfumo wa vyama vingi ulianzishwa nchini mnamo 1992 na licha ya nchi hii kufanya uchaguzi tangu 1962, bado kuna matatizo makubwa ya taasisi za kisiasa ambayo huifanya hali kuwa vigumu kumaliza uchaguzi bila mizozo. .[1]

Muundo wa Uchaguzi

[hariri | hariri chanzo]

Kenya hufdanya uchaguzi wa kitaifa, huku ikimchagua Kiongozi wa Nchi ambaye ni Rais na pia baraza la wabunge. Rais huchaguliwa na raia kwa kipindi cha miaka mitano. Bunge lina wabunge 224, 210 kati yao waliochaguliwa na raia kutoka katika kila jimbo la Uchaguzi kwa kipindi cha miaka mitano. 12 ni wabunge wateule.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Baada ya majadiliano na serikali ya Ukoloni ya Britain mnamo 1963, Serikali iliruhusu mfumo wa ‘’Kura moja kwa kila mmoja’’ mnamo 1963.[1] Uchaguzi wa kwanza uliisha taratibu huku Jomo Kenyatta akichaguliwa kama Waziri Mkuu wa kwanza wa Kenya mnamo 1963. Mwaka uliofuata, chama chake cha KANU ilihariri katiba ya Kenya kumfanya Kenyatta Rais wa kwanza wa Kenya[1] Chini ya uongozi wake, ushindani uliisha pole pole wakati vyama vya kisiasa vyote viliungana na, au kudhulumiwa na chama tawala cha KANU. ).[1]. Hii ilipelekea kuundwa kwa mfumo wa chama kimoja nchini mnamo hata baada ya kifo cha Jomo Kenyatta mnamo 1978. Kenya iligeuzwa rasmi kuwa nchi ya chama kimoja cha Kisiasa mnamo 1982 kufuatia mabadiliko ya katiba[1]. Baada ya maandamano ya Saba Saba mnamo 1990, KANU ilijikunja na kuanza mikakati ya kurekebisha mfumo wa kisiasa.[1] Mnamo 1992, kipengele ambacho kilikuwa kimeifanya Kenya kuwa na mfumo wa Chama Kimoja kilifutwa na Kenya ikarejea kuwa na Mfumo wa Vyama Vingi.[1]. Uchaguzi wa kwanza chini ya mfumo huo ulifanyika mnamo 1992 huku wa pili ukifanyika mnamo 1997. Katiba ya Kenya haikuwa imerekebishwa kutosha ili kuendeha mfumo huu. Hata hivyo, mnamo 2002, shughuli za uchaguzi zilitajwa kuwa za haki na huru na Jamii ya Kimaataifa, huku KANU ilkipokeza mamlaka kwa chama cha National Rainbow Coalition (NARC)[1]

Mfumo wa vyama Vingi tangu 1992

[hariri | hariri chanzo]
  1. Uchaguzi Mkuu wa Kenya, 1992
  2. Uchaguzi Mkuu wa Kenya, 1997
  3. Uchaguzi Mkuu wa Kenya, 2002
  4. Uchaguzi wa Urais wa Kenya, 2007
  5. Uchaguzi wa Bunge la Kenya, 2007

Uchaguzi wa Awali

[hariri | hariri chanzo]

Tazama Pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 The Electoral Process in Kenya: A Review of Past Experience and Recommendations for Reform (PDF) (Ripoti). International Foundation for Electoral Systems. 2008. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2011-09-27. Iliwekwa mnamo 2010-01-25. {{cite report}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help); line feed character in |title= at position 49 (help)

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]