Neptuni
Neptuni | |
---|---|
Neptuni yenye rangi halisi kama ilivyopigwa picha na Voyager 2. | |
Ugunduzi | |
Wagunduzi | |
Tarehe | 23 Septemba 1846 |
Jina | |
Asili ya jina | Kla. Neptūnus |
Majina mengine | Neptune (Kng.) |
Alama | |
Tabia za mzunguko | |
Mkaribio | km 4,460,000,000 au 29.81 |
Upeo | km 4,540,000,000 au 30.33 |
km 4,500,000,000 au 30.07 | |
Uduaradufu | 0.008678 |
siku 60,195 miaka 164.8 | |
Mwinamo | 1.770° toka njia ya Jua |
Miezi | 14 |
Tabia za maumbile | |
km 24,622±19 | |
Tungamo | kg 1.02413×1026 mara 17.147 ya Dunia |
g/cm3 1.638 | |
Uvutano wa usoni | m/s2 11.15 |
km/s 23.5 | |
siku 0.67125 | |
siku 0.6713 | |
Weupe | 0.290 (Bond) 0.442 (jiometri) |
Halijoto | K 72 (−201°C) |
Kwa elementi ya kikemia nenda Neptuni (elementi), kwa mungu wa Kiroma nenda Neptuni (kiasili)
Neptuni ni sayari ya nane kutoka Jua na ya nne kwa ukubwa wa kipenyo katika Mfumo wa Jua. Tungamo yake ni mara 17 ya ile ya Dunia. Pamoja na Mshtarii, Zohali na Uranusi, inahesabiwa kati ya sayari jitu za mfumo wetu.
Neptuni inazunguka Jua kwenye njiamzingo yake katika kipindi cha miaka 164.8 kwa umbali wa kilomita bilioni 4.5 au vizio astronomia 30.
Ugunduzi na jina
[hariri | hariri chanzo]Neptuni haionekani kwa macho matupu. Inawezekana ya kwamba Galileo Galilei, aliyekuwa mtu wa kwanza kutumia darubini kuangalia nyota, aliiona alipotazama anga lakini hakuitambua kama sayari, ila kama nyota mojawapo. Maana inasogea polepole sana kwenye anga kati ya nyota.
Neptuni ilitambuliwa katika karne ya 19 kutokana na makadirio ya kihisabati wakati wataalamu walitafuta maelezo ya kuchezacheza kwa sayari ya saba Uranusi katika obiti yake. Hapo kuwepo wa sayari ya nyongeza ulitabiriwa inayoathiri mwendo wa Uranusi. Hivyo ilitazamwa kwenye darubini kwa mara ya kwanza tarehe 23 Septemba 1846 karibu na mahali ilipotabiriwa.
Wavumbuzi mbalimbali walivutana kwa muda kuhusu jina na hatimaye mapendekezo ya kutumia jina la Neptunus, mungu wa Kiroma wa bahari, yalikubaliwa.
Tabia za sayari
[hariri | hariri chanzo]Habari nyingi kuhusu Neptuni zimepatikana kutokana na safari ya kipimaanga Voyager 2 iliyopita karibu nayo mwaka 1989.
Nusukipenyo chake ni kilomita 24,765 hivyo mara nne ya Dunia.
Muundo wa Neptuni unafanana na Uranus. Kuna kiini cha mwamba na metali chenye masi inayolingana takribani sawa na Dunia. Kiini hiki kinazungukwa na tabaka nene lenye mchanganyiko wa maji, amonia na methani katika hali ya kiowevu, kwa hiyo sehemu hii inaitwa pia bahari.
Juu yake ziko tabaka za angahewa inayofanywa na gesi kama hidrojeni, heli na methani. Hakuna tofauti kali kati ya sehemu za "angahewa" na "bahari" maana hali za mata zinaingiliana kutokana na shinikizo kubwa.
Tabaka za juu za angahewa ni baridi sana zikiwa na jotoridi ya nyuzi za K 55 (°C 218). Kitovu cha jotoridi kinapanda hadi kufikia takriban K 5,400 (°C 5,100).
Katika angahewa ya Neptuni zilipimwa dhoruba kali zinazofikia kasi ya zaidi ya kilomita 1600 kwa saa.
Neptuni huwa na mfumo wa bangili uliotambuliwa na Voyager 2.
Miezi
[hariri | hariri chanzo]Mwezi mkubwa unaitwa Tritoni uligunduliwa mwaka 1846, siku chache baada ya sayari yenyewe na kupokea jina lake kutokana na mwana wa mungu wa bahari katika mitholojia ya Kigiriki. Tritoni ina kipenyo cha kilomita 2707. Katika karne ya 20 miezi mingine ilitambuliwa inayozunguka Neptuni, hadi sasa jumla ni 14 lakini mingi ni midogo.
Kuiangalia sayari
[hariri | hariri chanzo]Neptuni huwa haionekani kwa urahisi: macho matupu hayawezi kuiona; ni lazima kutumia darubini, na hata hapo huonekana ikiwa imefifia kama kisahani chenye rangi ya buluu-kijani. Rangi hii imetokana na gesi ya methani inayopatikana kwa wingi katika angahewa yake. Kwa kutumia darubini kubwa, sayari huweza kuonekana kama kaduara kadogo chenye kipenyo cha kama sekunde za tao 2.3.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Wallah, W.B. & Mwamburi, J. Kiswahili mufti darasa la 8: Mwongozo wa mwalimu. Longhorn, 2009. ISBN 99966491066
- TESSA - Teacher Education in Sub Saharan Africa. Nishati na Mwendo: Kutoka Ardhini kenda kwenye nyota – kutumia Zana Kifani Archived 9 Aprili 2016 at the Wayback Machine.. Available at: www.tessafrica.net
- 3. Waweru, M.; Makombo, H; Vonuoli, A.; Kashihiri, C.; Mwayani, J.Hutua za Kiswahili: Masomo ya Msingi 8. East African Educational Publishers ltd., 1ed, 290p., 2005. ISBN 9966-25-403-X
- Maran, Stephen P. (2005). Astronomy for dummies, Inc. Wiley Publishing, Hoboken.
- Klimishin, Iwan A. (1991). Modern Astronomy, Akad. Verl Spektrum, Heidelberg.
- Birney, Scott D. (1991). Observational astronomy, Cambridge University Press, Cambridge.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- NASA Neptune Archived 25 Julai 2013 at the Wayback Machine.
- Sayari za Mfumo wa Jua Archived 13 Desemba 2006 at the Wayback Machine.
- Neptune katika wikipedia ya Kiingereza
- Voyager
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Neptuni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |