Mkoa wa Bagamoyo (DOA)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Jengo la Forodha, Bagamoyo 1913.

Mkoa wa Bagamoyo ilikuwa mkoa mmojawapo kati ya mikoa 21 ya koloni la Afrika ya Mashariki ya Kijerumani (DOA = Deutsch Ostafrika) lililokuwa mtangulizi wa nchi za Tanzania, Rwanda na Burundi wa leo.

Eneo na mipaka[hariri | hariri chanzo]

Mkoa huo ulikuwa na eneo la kilomita za mraba 14,200, kwa hiyo ilikuwa kati ya mikoa midogo zaidi ya koloni hii. Makao makuu (jer. Bezirksamt) yalikuwepo Bagamoyo mjini.

Mkoa wa kihistoria wa Bagamoyo (DOA) mnamo 1913 (na. IV).

Mkoa huu ulipakana na

Mkoa huo ulikuwa na ofisi ndogo (jer. Bezirksnebenstelle) pale Saadani.

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1913 kulikuwa na wakazi Waafrika 72,800, pamoja na Waasia (Wahindi, Waarabu hasa) 1,120 na Wazungu 64.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Mji wa Bagamoyo ulikuwa kitovu cha biashara, ingawa shughuli hizi ziliendelea kupungua (tazama chini). Kampuni mbalimbali zilikuwa na mashamba makubwa ambako pia kahawa na vanila zililimwa. Idadi ya walowezi Wazungu ilikuwa 4. Mwaka 1908 kampuni na walowezi Wazungu walikuwa na eneo la kilomita za mraba 435.

Kwenye mwaka 1913 takwimu ya Kijerumani ilihesabu ng'ombe 7,830, kondoo na mbuzi 17,800 na punda 326 kuwa mali ya wazalendo; Wazungu walifuga ng’ombe 1,065 na mbuzi/kondoo 145.

Mji na bandari ya Bagamoyo[hariri | hariri chanzo]

Bagamoyo yenyewe iliwahi kuwa mji muhimu wa Waswahili kabla ya ukoloni maana ilikuwa bandari kuu ya kutazama kisiwa cha Unguja. Hivyo ilikuwa bandari kuu upande wa bara tangu kupanuka kwa biashara ya misafara ya kuelekea Ziwa Tanganyika (Ujiji).

Mwanzoni ilikuwa mji mkuu wa koloni ingawa bandari yake haifai kwa meli zilizopaswa kukaa kilomita tatu mbele ya ufuko na kupokea au kutoa mizigo na abiria kupitia jahazi na vyombo vidogo. Bagamoyo ikaendelea kuwa mji muhimu wa biashara ya misafara hata baada ya uhamisho wa makao makuu ya koloni kwenda Dar es Salaam kuanzia mwaka 1891. Mnamo mwaka 1900 idadi ya wakazi ilikadiriwa kuwa mnamo 15,000.

Lakini tangu kuanzishwa kwa reli ya kati kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro (1907), halafu hadi Dodoma mwaka 1910 na hadi Tabora mwaka 1912 biashara ya misafara ilizidi kupungua pamoja na idadi ya watu walioishi Bagamoyo na mnamo mwaka 1913 walikuwa 5,000 tu.

Mwaka 1908 zilifika meli 149 na jahazi 698. Thamani ya bidhaa zilizopita Bagamoyo mwaka 1908 ilikuwa mark milioni 3.086. Mwaka 1912 idadi ya vyombo vya bahari kwa jumla ilikuwa 402 tu, na thamani ya bidhaa zilizopita hapa ilikuwa mark milioni 1.171. ? ilikuwa mark milioni 1.002.

Bagamoyo iliendelea kuwa na umuhimu wa pekee kwa sababu simu ya telegrafu kutoka Zanzibar ilifika hapa ikaendelea hadi Dar es Salaam ambayo wakati ule ilikuwa njia ya pekee ya mawasiliano ya haraka na dunia ya nje.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]