Nenda kwa yaliyomo

MV Nyerere

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ziwa la Viktoria Nyanza
Ziwa Viktoria Nyanza jinsi inavyoonekana kutoka angani
Ziwa Viktoria Nyanza jinsi inavyoonekana kutoka angani
Mahali Afrika ya Mashariki
Nchi zinazopakana Tanzania, Kenya na Uganda
Eneo la maji 68,100 km²
Kina cha chini 81 m
Mito inayoingia Kagera, Katonga, Nzoia
Mito inayotoka Nile
Kimo cha uso wa maji
juu ya UB
1,134 m
Miji mikubwa ufukoni Kampala, Kisumu, Mwanza

MV Nyerere ni jina la kivuko kilichokuwa kinafanya kazi zake katika Ziwa Viktoria nchini Tanzania ambapo tarehe 20 Septemba 2018 kilizama kikiwa kati ya visiwa vya Ukerewe na Ukara.[1][2]

MV Nyerere ilikuwa feri ndogo iliyotengenezwa mnamo mwaka 2004. Ilipangiwa kubeba tani 25 ya mizigo. Iliweza kusafirisha magari madogo matatu kama sehemu ya mzigo wake na abiria 100[3]. Ilihudumia mawasiliano kati ya kisiwa kikuu cha Ukerewe na kisiwa kidogo cha Ukara.

Wamiliki wa feri walikuwa Mamlaka ya Huduma za Umeme, Makanika na Elektroniki (TEMESA).[4] Shirika hilo lilikanusha kuwa kivuko cha MV Nyerere kilikuwa na matatizo ya kiufundi, na kuongeza kuwa kivuko hicho kilifanyiwa matengenezo makubwa mwezi uliopita ikiwa ni pamoja na matengenezo ya injini mbili za kivuko hicho.

Tukio la ajali

[hariri | hariri chanzo]

Kivuko cha MV Nyerere kilikuwa kikifanya safari zake kutoka Bugorora kwenda Ukara mnamo 20 Septemba 2018 kikiwa na abiria wanaokadiriwa kuwa 400 ndani ya chombo hicho; zaidi ya abiria hao inadaiwa kulikuwa na mizigo ya mahindi, ndizi na simenti (saruji).[1][5]

Inaaminika kuwa kivuko kilibeba zaidi ya abiria 400 wakati kilipokuwa kikizama pamoja na mizigo iliyopelekwa kwenda gulioni siku ile. Kwa hiyo idadi ya abiria ilikuwa takribani mara nne zaidi ya uwezo wa juu kabisa wa kivuko hicho.[4][1] Idadi kamili ya abiria waliokuwa wakisafiri kupitia kivuko hicho haijulikani kutokana na kupotea kwa kifaa cha kuhesabia watu wakati wa tukio la ajali hiyo.[6][2] Hadi siku tatu baada ya ajali serikali ya Tanzania ilitangaza kuwa watu zaidi ya 224 walipatikana wakiwa wamefariki dunia katika kivuko hicho ambapo idadi ya vifo ilihofiwa kufikia 300.[7]

Kivuko hicho kilianza kuzama umbali wa mita chache kabla ya kufika katika kituo kilipotakiwa kumaliza safari yake katika kisiwa cha Ukerewe.[2] Mashuhuda wa tukio hilo walieleza kuwa kiliegama upande mmoja na kupindukia ndani ya maji.[8] Maafisa wa Tanzania hawana uhakika bado na idadi kamili ya abiria waliokuwemo ndani ya chombo hicho kutokana na mhusika wa kugawa na kutunza tiketi za kusafiria katika chombo hicho kuzama, na pia mashine ya kurekodi idadi ya abiria kupotea katika purukushani hiyo.[5][6] Taarifa kinzani zilitoa makadirio kivuko hicho kilikuwa kikibeba watu zaidi ya 300, [8] wakati taarifa nyingine zikisema kivuko kilibeba watu zaidi ya 400.[1]

Polisi na Serikali walithibitisha kuokolewa kwa watu41 baada ya tukio hilo, amabapo zoezi la uokoaji liliahirishwa mpaka kesho yake.[9]

Siku iliyofuata, wakati wa mkutano na vyombo vya habari kuhusu ajali hiyo, Rais wa Tanzania John Magufuli alitangaza idadi ya vifo ilikuwa 131, na wengine 40 waliweza kuokolewa na kupelekwa ufukweni salama.[10] Kama sehemu ya zoezi la uokoaji, polisi kwa kushirikiana na jeshi la wanamaji walipelekwa eneo la tukio ili kutafuta watu ambao bado walikuwa hawajapatikana.[11] Hata hivyo, kutokana na kuwepo kwa idadi ya abiria ambao bado walikuwa hawajatambuliwa walipo, idadi ya vifo ilihofiwa kufikia zaidi ya 200.[12]

Mnamo tarehe 23 Septemba 2018 (siku tatu baada ya tukio la ajali kutokea) rais John Magufuli alitangaza tena kuwa idadi ya vifo ilikuwa imefikia 224, na alisisitiza uamuzi wake wa awali wa kukamatwa kwa menejimenti iliyohusika na tukio hilo ikiwa ni pamoja na kukamatwa kwa nahodha wa chombo hicho.[7]

Mwitikio wa jamii

[hariri | hariri chanzo]

Magufuli alielezea kusikitishwa kwake na hivyo kutangaza siku 4 za maombolezo ya Kitaifa kufuatia ajali hiyo mbaya ya kupinduka kwa kivuko hicho.[13] Pia aliamuru kukamatwa kwa menejimenti iliyohusika na kivuko hicho akiwatuhumu kwa uzembe wa kuzidisha mizigo katika chombo hicho ikilinganishwa na uwezo wa chombo chenyewe ambapo ilielezwa kuwa chombo kilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 101.[14][6]

Mwanasiasa wa upande wa upinzani John Mnyika, wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), aliituhumu serikali kwa kushindwa kuhakikisha ubora wa vyombo vya majini na kusuasua kwa zoezi la uokoaji.[15][16]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 "Dozens drown in Lake Victoria capsizing", BBC News, 20 September 2018. (en-GB) 
  2. 2.0 2.1 2.2 "Over 200 feared dead as ferry capsizes in Tanzania". RTÉ. 20 Septemba 2018. Iliwekwa mnamo 21 Septemba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Tanzania: Dar Plunges Into Mourning, MV Nyerere Death Toll, tovuti ya allafrica.com ya 22 Septemba 2018, iliangaliwa 24-09-2018
  4. 4.0 4.1 "At least 136 bodies recovered after ferry capsizes in Tanzania". The Irish Times. 20 Septemba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. 5.0 5.1 Staff and agencies (20 Septemba 2018). "More than 200 feared drowned in Tanzania ferry disaster". The Guardian (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 20 Septemba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. 6.0 6.1 6.2 Burke, Jason (21 Septemba 2018). "Tanzania's president orders arrests as ferry death toll climbs". The Guardian.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. 7.0 7.1 "Tanzania buries ferry disaster dead as toll hits 224". Times Live. 23 Septemba 2018. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-12-25. Iliwekwa mnamo 2018-09-23.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; name "Times Live" defined multiple times with different content
  8. 8.0 8.1 "Ferry capsizes on Tanzania’s Lake Victoria, killing dozens", France 24, 20 September 2018. (en-US) 
  9. "Tanzania ferry capsize: Dozens killed as rescue effort suspended", www.aljazeera.com. Retrieved on 21 September 2018. 
  10. "Lake Victoria Tanzania ferry disaster: Divers hunt for survivors". BBC. 21 Septemba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. "Death toll reaches 136 in Tanzania ferry disaster with scores missing". Reuters. 21 Septemba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  12. "Lake Victoria, Tanzania ferry disaster death toll doubles". BBC News. 21 Septemba 2018. Iliwekwa mnamo 21 Septemba 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  13. "Magufuli orders arrest of MV Nyerere operator", Daily Nation. Retrieved on 21 September 2018. (en-UK) 
  14. "Magufuli: The person steering MV Nyerere ferry was un-trained", The Citizen, 21 September 2018. Retrieved on 21 September 2018. (en) 
  15. "Tanzania ferry disaster: 136 bodies pulled from Lake Victoria", the Guardian, 21 September 2018. Retrieved on 21 September 2018. (en) 
  16. "Plea of lawmaker who predicted MV Nyerere tragedy", The Citizen, 21 September 2018. Retrieved on 21 September 2018. (en) 

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu MV Nyerere kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.