Laurenti Mfiadini





Laurenti (kwa Kilatini "Laurentius", Valencia au Huesca, Hispania, 225 hivi - Roma, Italia, 10 Agosti 258) alikuwa shemasi mkuu wa Kanisa la Roma hadi alipouawa kwa kubanikwa kutokana na imani yake katika Yesu.
Laurenti alikuwa msimamizi wa mali ya Kanisa la Roma iliyotumiwa kwa ajili ya kuwasaidia maskini. Serikali ya Kaisari Valerian iliwahi kumwua askofu wa Roma Sixtus II ikadai sasa Laurenti atoe hazina yote ya Kanisa kwa serikali ya Kaisari katika muda wa siku tatu. Laurenti alitumia muda huo kugawa pesa zote kwa maskini. Siku alipotakiwa kufika mbele ya afisa wa serikali kukabidhi pesa alikuja pamoja na kundi kubwa cha maskini, wagonjwa, walemavu, vipofu, wenye ukoma, wajane na mayatima. Alimwambia akida, "Hao ndio hazina ya Kanisa". Akida alimtesa na kumfunga kwenye nondo za chuma juu ya moto hadi alikufa. Inasemekana ya kwamba Laurenti alivumulia mateso kimyakimya akisema mwishoni, "Ewe mtu maskini, kwangu moto huu umepoa lakini kwako utaleta maumivu ya milele"
Anaheshimiwa na madhehebu mbalimbali ya Ukristo kama mtakatifu mfiadini, hasa siku ya kifodini chake[1].
Tazama pia[hariri | hariri chanzo]
- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi[hariri | hariri chanzo]
Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]
- Henry Wace, A Dictionary of Christian Biography Archived 18 Mei 2008 at the Wayback Machine.: Laurentius
- Catholic Encyclopedia Saint Lawrence
- Golden Legend: Archived 29 Oktoba 2005 at the Wayback Machine. "The Life of Saint Laurence"
- Leo I: Sermon on St Lawrence
- Orthodox Christianity Church of Saint Lawrence
- [1] Archived 14 Februari 2012 at the Wayback Machine. Church of Saint Lawrence, Birgu, Malta
![]() |
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |