Kaizari Valerian
Mandhari
(Elekezwa kutoka Valerian)
Publius Licinius Valerianus (takriban 193/200 – 260/264) alikuwa Kaizari wa Dola la Roma kuanzia tarehe 22 Oktoba 253 hadi 260 alipotekwa na mfalme Shapur I wa Uajemi. Jambo hilo jipya lilitikisa dola lote.
Wakati alipoandaa vita yake dhidi ya Uajemi aliamuru sadaka kwa miungu ya Roma zitolewe pia na Wakristo. Aliposikia kwamba walikataa aliagiza kuua maaskofu; Wakristo wengine waliokuwa na cheo walipoteza cheo na mali na kuuzwa kama watumwa wakikataa sadaka hiyo[1]. Alitawala pamoja na mwana wake, Kaizari Galienus. Baada ya kifo cha baba yake, Galienus alisimamisha dhuluma dhidi ya Wakristo. Alimfuata Aemilianus.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ W. H. C. Frend (1984). The Rise of Christianity. Fortress Press, Philadelphia. p. 326. ISBN 978-0800619312.
Makala hii kuhusu Kaizari fulani wa Roma bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kaizari Valerian kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |