Gregori Barbarigo
Gregori Yohane Barbarigo (Venezia, leo nchini Italia, 16 Septemba 1625 – Padova, 17 Juni 1697) alikuwa askofu na kardinali.
Papa Klementi XIII alimtangaza mwenye heri tarehe 16 Julai 1761 na Papa Yohane XXIII mtakatifu tarehe 26 Mei 1960.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Muda mfupi baada ya upadrisho (21 Desemba 1655) aliitwa na Papa Aleksanda VII mjini Roma akafanywa mwenyekiti wa kamati ya kuhudumia waliopatwa na tauni. Hapo alijitosa kuwatembelea, kuwasaidia na kuwazika mwenyewe.
Mwaka uliofuatwa alifanywa askofu wa Bergamo. Alikataa mashangilio, akaagiza pesa ambazo zingetumika zigawiwe kwa fukara. Halafu mwenyewe aliuza mali yake yote kuwasaidia.
Tarehe 5 Aprili 1660 alifanywa kardinali.
Tarehe 24 Machi 1664 alihamishiwa jimbo la Padova ambalo aliliongoza miaka 33 akitembelea parokia zote 320.
Mkarimu kwa wote na mgumu kwake mwenyewe, alianzisha seminari kwa malezi ya miito na shule nyingi, alifundisha katekisimu kwa watoto katika kilugha chao, aliendesha sinodi ya kijimbo na kujadiliana na mapadri wake [2].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Mabradha wa Shule za Kikristo
- Orodha ya Watakatifu Waaugustino
- Orodha ya Watakatifu Wabazili
- Orodha ya Watakatifu Wabenedikto
- Orodha ya Watakatifu Wadominiko
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
- Orodha ya Watakatifu Wajesuiti
- Orodha ya Watakatifu Wakarmeli
- Orodha ya Watakatifu Wakolumbani
- Orodha ya Watakatifu Wamersedari
- Orodha ya Watakatifu Waoratori
- Orodha ya Watakatifu Wapasionisti
- Orodha ya Watakatifu Wapremontree
- Orodha ya Watakatifu Waredentori
- Orodha ya Watakatifu Wasalesiani
- Orodha ya Watakatifu Waskolopi
- Orodha ya Watakatifu Wateatini
- Orodha ya Watakatifu Watrinitari
- Orodha ya Watakatifu Watumishi wa Maria
- Orodha ya Watakatifu Wavinsenti
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Martyrologium Romanum, Libreria Editrice Vaticana (2001), ISBN 88-209-7210-7
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/58050
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Hagiography Circle Ilihifadhiwa 28 Agosti 2017 kwenye Wayback Machine.
- St. Catholic Online
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |