Chelsea F.C.
Picha:Chelsea FC.svg | |||
Jina kamili | Chelsea Football Club | ||
---|---|---|---|
Jina la utani | The Pensioners, The Blues | ||
Imeanzishwa | Machi 10, 1905 | ||
Uwanja | Stamford Bridge (Uwezo: 41,841) | ||
Mmiliki | Roman Abramovich -pending | ||
Mwenyekiti | Bruce Buck | ||
Meneja | Thomas Tuchel | ||
Ligi | Premier League | ||
2021-22 | Premier League, 3th | ||
|
Chelsea Football Club[1][2] [3][4]ni klabu ya mpira wa miguu ya nchini Uingereza iliyo na maskani yake Fulham, London. Klabu hii ilianzishwa mwaka 1905, na kwa miaka mingi sana imekuwa ikishiriki ligi kuu ya Uingereza. Uwanja wao wa nyumbani ni Stamford Bridge ambao una uwezo wa kuingiza watazamaji 41,837, wameutumia uwanja huu tangu klabu ilivyoanzishwa.
Chelsea, kwa mara ya kwanza ilipata mafanikio makubwa mwaka 1955, ambapo walipata ubingwa wa ligi, na walishinda mataji kadhaa katika miaka ya 1960, 1970, 1990 na 2000. Klabu hii imefurahia zaidi mafanikio katika miongo miwili ilopita, kwa kushinda mataji makubwa 15 tangu mwaka 1997.
Nyumbani, Chelsea imeshinda ubingwa wa ligi mara nne, kombe la FA mara saba, kombe la ligi mara nne, pamoja na ngao za jamii mara nne. Na kimataifa Chelsea imeshashinda UEFA Cup Winners' Cups mara mbili, UEFA Super Cup moja, UEFA Europa League moja na UEFA Champions League moja. Chelsea ndio klabu pekee kutoka London kushinda UEFA Champions League, na ni moja kati ya klabu nne kutoka Uingereza, kuchukua makombe yote makubwa matatu ya Ulaya.
Kwa kawaida Chelsea huvaa jezi ya blu, kaptula blu na soksi nyeupe. Nembo ya klabu imebadilishwa mara nyingi kulingana na wakati na kuboresha muonekano wa klabu. Nembo ya sasa inaonesha picha ya simba akiwa amebeba mkuki. Tangu Julai 2003, Chelsea imekuwa ikimilikiwa na Bilionea wa Kirusi, Roman Abramovich.
Wachezaji[hariri | hariri chanzo]
- As of 7 January 2018.[5]
Note: Flags indicate national team as has been defined under FIFA eligibility rules. Players may hold more than one non-FIFA nationality.
|
|
Tuzo[hariri | hariri chanzo]
- Ligi Kuu (6) 1954-1955, 2004-2005, 2005-2006, 2009-2010, 2011-2012, 2016-2017
- FA Cup (7) 1970, 1997, 2000, 2007, 2009, 2010, 2018
- Kombe la Ligi (4) 1965, 1998, 2005, 2007;
- Ngao ya Jamii (4) 1955, 2000,2005, 2009
- UEFA Cup Winners' Cup (2) 1971, 1998
- UEFA Super Cup (1) 1998, 1999, 2003
- Full Members Cup (2) 1986, 1990
- FA Youth-cup (3) 1960, 1961, 2010
Tanbihi[hariri | hariri chanzo]
- ↑ Danyal Khan, Jake Stokes (2022-05-03). Chelsea news and transfers LIVE: Todd Boehly takeover hint, Abramovich fear (en). Football.London. Iliwekwa mnamo 2022-05-03.
- ↑ Bobby Vincent (2022-05-03). Chelsea could look to reunite Lautaro Martinez and Romelu Lukaku in the summer (en). Football.London. Iliwekwa mnamo 2022-05-03.
- ↑ Luke Thrower (2022-05-04). Glen Johnson urges Chelsea to offer Jorginho a new contract amid transfer links (en). Football.London. Iliwekwa mnamo 2022-05-04.
- ↑ Luke Thrower (2022-05-04). Chelsea bidder Lord Coe warns club to find quick takeover solution (en). Football.London. Iliwekwa mnamo 2022-05-04.
- ↑ First Team Squad List. Chelsea F.C. Iliwekwa mnamo 7 August 2018.