Nenda kwa yaliyomo

Mbuzi-kaya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Capra aegagrus hircus)
Mbuzi-kaya
Mbuzi na mwanawe
Mbuzi na mwanawe
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Artiodactyla (Wanyama wenye vidole viwili au vinne mguuni)
Nusuoda: Ruminantia (Wanyama wanaocheua)
Familia: Bovidae (Wanyama walio na mnasaba na ng'ombe)
J. E. Gray, 1821
Nusufamilia: Caprinae (Wanyama wanaofanana na mbuzi)
Jenasi: Capra (Mbuzi)
Linnaeus, 1758
Spishi: C. aegagrus (Mbuzi-mwitu)
Erxleben, 1777
Nususpishi: C. a. hircus (Mbuzi-kaya)
(Linnaeus, 1758)
Mbuzi akikamuliwa maziwa.

Mbuzi-kaya ni mnyama katika ngeli ya mamalia ambaye huzaa na kunyonyesha mwenye miguu minne na mwenye tabia zinazofanana na ng'ombe. Kwa ukubwa, mbuzi aliyekomaa ni pungufu ya theluthi moja ya ng'ombe aliyekomaa.

Mbuzi-kaya, kama alivyo n'gombe, ni mnyama anayefugika. Hufugwa kwa ajili ya nyama, maziwa na ngozi yake. Kwani nyama na maziwa ni chakula, na ngozi kufanywa viatu, mishipi na mikoba pia.

Mbuzi-kaya hula majani, hucheua na kutafuna tafuna chakula chake mara kadhaa ilhali kikizunguka kati ya vyumba mbalimbali vya tumbo na mdomo wake kabla ya kukimeza kabisa, kama vile afanyavyo ng'ombe.

Mara nyingi mbuzi-kaya hubeba mimba na kuzaa mapacha kadhaa.

Mbuzi ni kati ya wanyama wa kwanza waliofugwa na binadamu. Kuna spishi za kufugwa na spishi za porini.

Faida za mbuzi

[hariri | hariri chanzo]

Kuna faida nyingi za mbuzi aina hizo ni:

  • (i) Hutupatia ngozi kwa ajili ya kutengenezea vitu kama viatu.
  • (ii) Hutupatia nyama.
  • (iii) Hutupatia kwato kwa ajili ya kutengenezea vitu kama vishikizo vya nguo.
  • (iv) Hutupatia maziwa.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mbuzi-kaya kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Lua error in package.lua at line 80: module 'Module:Navbar/configuration' not found. Ili kupata maelezo kuhusu masanduku ya uanapwa ya spishi angalia: Wikipedia:WikiProject Mammals/Article templates/doc.