Saint Vincent na Grenadini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Saint Vincent and the Grenadines
Bendera ya Saint Vincent na Grenadini Nembo ya Saint Vincent na Grenadini
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Pax et justitia
(Kilatini: Amani na haki)
Wimbo wa taifa: St Vincent Land So Beautiful
Lokeshen ya Saint Vincent na Grenadini
Mji mkuu Kingstown
13°10′ N 61°14′ W
Mji mkubwa nchini Kingstown
Lugha rasmi Kiingereza
Serikali Demokrasia
Nchi ya Jumuiya ya Madola
Charles III wa Uingereza
Susan Dougan
Ralph Gonsalves
Uhuru
tarehe

27 Oktoba 1979
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
389 km² (ya 201)
Kidogo sana
Idadi ya watu
 - [[2021]] kadirio
 - [[2021|2021]] sensa
 - Msongamano wa watu
 
104,332 (ya 179)
100.455
307/km² (ya 39)
Fedha East Caribbean dollar (XCD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC-4)
(UTC)
Intaneti TLD .vc
Kodi ya simu +1-784

-


Ramani ya St. Vincent na Grenadini

Saint Vincent na Grenadini ni nchi ya visiwani ya Antili Ndogo katika bahari ya Karibi. Iko kaskazini kwa Grenada na Trinidad na Tobago na kusini kwa Saint Lucia.

Saint Vincent ndiyo kisiwa kikubwa na Grenadini ni kundi la visiwa vidogo. Kwa jumla eneo la nchi kavu ni kilometa mraba 389.

Mji mkuu wa Kingstown, huko St. Vincent.

Watu[hariri | hariri chanzo]

Wakazi wengi wana asili ya Afrika (66%) au ni machotara (19%). 6% ni Wahindi, 4% Wazungu (hasa wenye asili ya Ureno) na 2% Waindio ambao ndio wenyeji wa Karibi.

Lugha rasmi ni Kiingereza, lakini wananchi wengi wanaongea kwa kawaida Krioli

Upande wa dini, walio wengi (88.6%) ni Wakristo wa madhehebu mbalimbali, kuanzia Waanglikana na Wapentekoste, halafu Wamethodisti, Waadventista Wasabato, Wabaptisti na Wakatoliki. Wahindu ni 3.4%, Warastafari 1.8%, Baha'i 1.6, Waislamu 1.5% n.k.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Saint Vincent na Grenadini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.