Mkoa wa Ruvuma
Mkoa wa Ruvuma |
|
Mahali pa Mkoa wa Ruvuma katika Tanzania | |
Majiranukta: 11°0′S 36°0′E / 11.000°S 36.000°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Wilaya | 8 |
Mji mkuu | Songea |
Serikali | |
- Mkuu wa Mkoa | Christine G. Ishengoma |
Eneo | |
- Jumla | 63,498 km² |
Idadi ya wakazi (2022) | |
- Wakazi kwa ujumla | 1,848,794 |
Tovuti: http://www.ruvuma.go.tz/ |
Mkoa wa Ruvuma ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania.
Umepewa jina kutokana na mto Ruvuma ambao ni mpaka wake wa kusini na Msumbiji. Umepakana na Ziwa Nyasa na Mkoa wa Morogoro upande wa magharibi, mikoa ya Iringa na Lindi upande wa kaskazini na Mkoa wa Mtwara upande wa mashariki.
Makao makuu ya mkoa yako Songea mjini.
Wilaya
[hariri | hariri chanzo]Ndani ya mkoa huo kuna wilaya nane ambazo ni (katika mabano idadi ya wakazi mwaka 2022[1]):
- Nyasa (191,193)
- Songea Mjini (286,285),
- Songea Vijijini (178,201),
- Tunduru (412,054),
- Madaba (65,215),
- Mbinga Vijijini (285,582),
- Mbinga Mjini (158,896),
- Namtumbo (271,368).
Wakazi
[hariri | hariri chanzo]Jumla ya wakazi wote katika Mkoa wa Ruvuma ni 1,848,794 (sensa ya mwaka 2022).
Makabila makubwa katika Ruvuma ni Wangoni, Wamatengo, Wayao, Wandendeule, Wamanda, Wanyasa, Wapoto, Wabena na Wandengereko.
Karibu na Songea iko monasteri kubwa ya Peramiho ya watawa Wabenedikto na nyingine iko Hanga.
Elimu
[hariri | hariri chanzo]Elimu bado inahitajika, hasa kwa maeneo ya vijijini, maana watu wengi katika mkoa huu hawajaelimika hivyo huleta changamoto katika maendeleo maana taifa huhitaji watu ambao ni wasomi.
Miundombinu
[hariri | hariri chanzo]Sehemu ya mashariki ya mkoa kuna barabara ya lami kutoka Dar es Salaam kupitia Makambako na Njombe hadi Songea. Barabara kuu kwenda Lindi ni kiwango cha lami kuanzia Songea mjini kupitia Wilaya za Namtumbo, Tunduru, Nanyumbu, Masasi, Mnazimmoja-Lindi, hadi Dar es Salaam.
Majimbo ya bunge
[hariri | hariri chanzo]Wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015 mkoa huu ulikuwa na majimbo ya uchaguzi yafuatayo:
- Songea Mjini : mbunge ni Leonidas Tutubert Gama (CCM)
- Nyasa : mbunge ni Stella Manyanya (CCM)
- Tunduru Kaskazini : mbunge ni Ramo Matala Makani (CCM)
- Tunduru Kusini : mbunge ni Daimu Iddi Mpakate (CCM)
- Peramiho : mbunge ni Jenista Mhagama (CCM)
- Madaba : mbunge ni Joseph Kisito Mhagama (CCM)
- Namtumbo : mbunge ni Edwin Amandus Ngonyani (CCM)
- Mbinga Mjini : mbunge ni Sixtus Mapunda (CCM)
- Mbinga Vijijini : mbunge ni Martin Msuha (CCM)
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tovuti ya Mkoa wa Ruvuma
- (Kiingereza) Matokeo ya sensa 2002: Ruvuma Region Homepage for the 2002 Tanzania National Census
- Tanzanian Government Directory Database
- (Kiingereza) Makabila ya Tanzania
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Geita | Iringa | Kagera | Katavi | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Njombe | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Simiyu | Singida | Songwe | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Ruvuma bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Ruvuma kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |