Peramiho
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Peramiho ni jina la tarafa katika mkoa wa Ruvuma, wiliya ya Songea Vijijini panapojulikana kutokana na abasia ya wamonaki wakatoliki Wabenedikto.
Abasia hii ilianzishwa kama kituo cha umisionari na P. Cassian Spiss O.S.B. aliyefika Peramiho mwaka 1898. Mnamo mwaka 1931 Peramiho ilifanywa kuwa abasia na pia makao ya jimbo chini ya Abate-Askofu Gallus Steiger O.S.B.. Makao ya jimbo yalihamishiwa Songea mnamo mwaka 1969, na siku hizi kuna majimbo matatu (Songea, Njombe na Mbinga) yaliyotokana na jimbo la zamani la Peramiho.
Peramiho kuna shule na hospitali nzuri pamoja na monasteri.