Makambako

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Mji wa Makambako
Mji wa Makambako is located in Tanzania
Mji wa Makambako
Mji wa Makambako

Mahali pa Makambako katika Tanzania

Majiranukta: 8°51′S 34°50′E / 8.850°S 34.833°E / -8.850; 34.833
Nchi Tanzania
Mkoa Njombe
Wilaya Mji wa Makambako
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 146,481
Makambako.

Makambako ni mji na wilaya katika Mkoa wa Njombe, Tanzania, yenye postikodi namba 59113.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 146,481 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata 8 za Makambako zilikuwa na jumla ya wakazi 93,827[2] walioishi humo.

Hadi mwaka 2012 Makambako yenyewe ilikuwa kata ya Wilaya ya Njombe katika Mkoa wa Iringa. Kwa sasa ni mji wenye hadhi ya halmashauri ukiwa ni kitovu cha biashara mbalimbali na kilimo yakiwamo mazao ya mbao na nafaka.

Makambako ni njiapanda muhimu kusini mwa Tanzania. Barabara za TANZAM (Dar es Salaam - Mbeya) na barabara ya kuelekea Songea - Mtwara zinakutana huko, pamoja na kituo cha reli ya TAZARA.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. Sensa ya 2012, Njombe - Makambako TC. Jalada kutoka ya awali juu ya 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2017-03-29.
Kata za Wilaya ya Makambako Mjini - Mkoa wa Njombe - Tanzania

Kitandililo | Kitisi | Kivavi | Lyamkena | Maguvani | Mahongole | Majengo | Makambako | Mjimwema | Mlowa | Mwembetogwa | Ubena | Utengule


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Njombe bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Makambako kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.