Kipindupindu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Kipindupindu ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria aitwaye Vibrio cholerae. Maambukizi ya ugonjwa huu ni kwa kula au kunywa chakula chenye bakteria Vibrio cholerae inatotoka kwa wagonjwa wenye maradhi ya Kipindupindu. Dalili za ugonjwa huu ni homa kali na kuendesha.

Bakteria wa Vibrio cholerae

[1][2]

Vifo kutokamana na ugonjwa huu katika bara Afrika ni takriban 5%.

Matibabu[hariri | hariri chanzo]

Hospitali mjini Dhaka inayoonyesha vitanda vya wanaougua ugonjwa wa kipindupindu

1. Mgonjwa hunyweshwa maji mengi, kwa ajili mwili wake hupoteza maji mengi anapougua maradhi haya.

2. Dawa zinazojulikana kufanya kazi ni kama cotrimoxazole, erythromycin, doxycycline, chloramphenicol, na furazolidone.[3] 3. Chanjo za kuzuia Kipindipindu hutolewa katika baadhi za nchi.[4]

Kuepuka kupata Kipindupindu[hariri | hariri chanzo]

 • Maji ya choo yanayotokamana na wagonjwa wa maradhi ya kipindupindu yanapasa kupitia shimo za choo zilizohifadhiwa vizuri ili kuzuia usanbazaji wa bakteria. Vifaa vyote vinavyotumiwa na wagonjwa vinapaswa kuchemshwa kwa maji ya moto. Mikono inayoshika wagonjwa au nguo zao yanapaswa kuoshwa kwa sabuni.
 • Mashimo ya choo yanapaswa kutiwa dawa za kuuwa bakteria kwa kutumia klorini.
 • Maji yanafaa kuchemshwa kabla ya kutumiwa.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka 1816-1826 ndio kulikuwa na janga la kwanza la kipindupindu mjini Bengal, nchini India. Waingereza 10,000 na wenyeji India walikufa.[5]

Janga la pili la kipindupindu lilikuwa mnamo 1829-1851 iliyoenea nchini Urusi, Hungaria, Ujerumani na London. Zaidi ya watu 55,000 walikufa kutoka Uingereza.[6] Mwaka wa 1831, watu 150,000 walikufa kutokana na janga hili nchini Misri.[7]

Mwaka wa 1849, kipindupindu ilizuka tena kwa mara ya pili mjini Paris.[8] Mjini London, watu 14,137 walikufa.

Miaka ya 1961-1970: kulikuwa na janga lingine la kipindupindu nchini Indonesia. Ilianzia Afrika Kaskazini na kuenea hadi nchi ya Italia. Katika miaka ya 1970, watu kidogo waliathirika nchini Ujapani.

Mnamo 1991-1994 kulikuwa na janga lingine nchini Marekani ya Kusini, iliyosababishwa na meli iliyomwaga maji machafu. Mjini Peru, watu takriban 10,000 waliuawa.

Mwaka wa 2000, wagonjwa 14000 waliripotiwa kuugua kutokana na kipindupindu. Takriban 87% waliripotiwa kutoka bara la Afrika.[9]

Julai - Desemba 2007: ukame wa maji safi ya kunywa nchini Irak ilisababisha janga la Kipindupindu.[10] Watu 22 walifariki.[11]

Mnamo Agosti 2007 mjini Orissa, India. Zaidi ya watu 2,000 walilazwa hospitalini.[12]

Machi - Aprili 2008: Watu 2,490 walilazwa hospitalini mjini Vietnam kutokamana na janga la kipindupindu.[13]

Waathirika Maarufu[hariri | hariri chanzo]

George Bradshaw Nicolas Léonard Sadi Carnot Charles X of France Juan de Veramendi John Blake Dillon Alexandre Dumas, père, mwandishi wa Kifaransa aliyeandika kitabu cha The Three Musketeers Mary Abigail Fillmore, mtoto wa rais wa Marekani: Millard Fillmore James K. Polk, rais wa kumi na moja wa Marekani Pedro V, Mfalme wa nchi ya Portugal

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. Ryan KJ, Ray CG (editors) (2004). Sherris Medical Microbiology, 4th, McGraw Hill, 376–7. ISBN 0838585299. 
 2. Faruque SM; Nair GB (editors) (2008). Vibrio cholerae: Genomics and molecular biology. Caister Academic Press. ISBN 978-1-904455-33-2. 
 3. Cholera treatment. Molson Medical Informatics (2007). Iliwekwa mnamo 2008-01-03.
 4. Is a vaccine available to prevent cholera?. CDC disease info: Cholera. Iliwekwa mnamo 2008-07-23.
 5. The 1832 Cholera Epidemic in New York State, By G. William Beardslee.
 6. Asiatic Cholera Pandemic of 1826-37.
 7. Cholera Epidemic in Egypt (1947).
 8. The Irish Famine.
 9. Disease fact sheet: Cholera. IRC International Water and Sanitation Centre.
 10. "U.N. reports cholera outbreak in northern Iraq", CNN. Retrieved on 2007-08-30. 
 11. Cholera crisis hits Baghdad, The Observer, 2 Desemba 2007.
 12. Cholera death toll in India rises, BBC News.
 13. Cholera Country Profile: Vietnam. WHO.