Jimbo Katoliki la Kayanga
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jimbo Katoliki la Kayanga (kwa Kilatini Dioecesis Kayangana) ni mojawapo kati ya majimbo 33 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.
Kikanisa linahusiana na jimbo kuu la Mwanza.
Askofu wake wa kwanza ni Almachius Vincent Rweyongeza.
Yaliyomo |
Historia [hariri]
- 1929: Kuanzishwa kwa Apostolic Vicariate ya Rulenge-Ngara kutokana na Apostolic Vicariate ya Tabora
- 25 Machi 1953: Rulenge kufanywa dayosisi
- 14 Agosti 2008: Kumegwa dayosisi ya Rulenge na kuanzishwa jimbo jipya la Kayanga
Uongozi [hariri]
- Askofu Almachius Vincent Rweyongeza (tangu mwanzo).
Takwimu [hariri]
Eneo ni la kilometa mraba 13,004, ambapo kati ya wakazi 438,093 (2008) Wakatoliki ni 280,000 (63.9%).
Mapadri ni 25, hivyo kwa wastani kila mmojawao anahudumia waamini 11,200 katika parokia 11.
Masista ni 45.
Viungo vya nje [hariri]
- Catholic Hierarchy
- Giga Catholic
- Hati Congregatio pro Gentium, AAS 100 (2008), uk. 597