Yosefu Oriol

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu ya Mt. Josep Oriol - Basilica de Santa Maria del Mar, Barcelona, Hispania.
Kaburi la Mt. Yosefu Oriol.

Yosefu Oriol (kwa Kikatalunya Sant Josep Oriol; kwa Kihispania José Orioli) (Barcelona, 23 Novemba 1650 – Barcelona 23 Machi 1702) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki na mwanachama wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko nchini Hispania.

Tangu wakati wa uhai wake amejulikana kama "Mtendamiujiza wa Barcelona"

Papa Pius VII alimtangaza mwenye heri tarehe 5 Septemba 1806, halafu Papa Pius X alimfanya mtakatifu tarehe 20 Mei 1909.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 23 Machi[1]

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Mzaliwa wa Barcelona, alisoma katika chuo kikuu cha mji huo, akapata udaktari wa teolojia tarehe 1 Agosti 1674.

Alipewa upadrisho tarehe 30 Mei 1676.

Alitembelea Roma mwaka 1686 akapewa cheo katika kanisa la Santa Maria del Pi mjini Barcelona, ambapo amezikwa.

Akitamani kuwa mfiadini, alisafiri kwenda Roma mnamo Aprili 1698 ili ajitolee kwenda umisionari, lakini akaugua huko Marseille akarudi Barcelona.

Alijulikana kwa maisha ya kujitesa, ufukara na sala ya kudumu akiwa amejaa furaha ya Kimungu akasemekana kuwa na karama za unabii na uponyaji wa mara moja.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.