WikiIndaba 2017

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Logo ya WikiIndaba 2017

Wikiindaba 2017 ulikuwa mkutano wa taasisi ya Wikimedia Foundation kwa ajili ya Afrika uliofanyika mjini Accra (Ghana) tarehe 10 - 22 Januari 2017. Waliokaribishwa ni wachangiaji wa Wikipedia na miradi mingine ya maarifa huria kutoka nchi za Afrika pamoja na maafisa wa ofisi kuu ya Wikimedia. Shabaha ilikuwa kuimarisha mawasiliano kati ya washiriki na hali ya media huria barani Afrika.

Jina[hariri | hariri chanzo]

WikiIndaba ni neno lililoundwa na "Wiki" kwa "Wikipedia / Wikimedia" na "Indaba" ambalo ni neno la lugha ya Kizulu yenye maana ya "mkutano, ushauri wa pamoja'. Ilikuwa WikiIndaba ya pili baada ya mkutano wa kwanza uliotokea Afrika Kusini mwaka 2014.

Waliohudhuria[hariri | hariri chanzo]

Wanamkutano huko Accra 2017

Kwa jumla walihudhuria mkutano watu 50 kutoka nchi 13 za Afrika (Afrika Kusini, Algeria, Botswana, Côte d'Ivoire, Ghana, Kamerun, Kenya, Moroko/Uswidi, Misri, Namibia, Nigeria, Tunisia na Uganda), mjumbe wa Wikipedia ya Kiswahili pamoja na wageni kutoka Wikimedia Ujerumani na maafisa wa Wikimedia kutoka Marekani. Wageni wengine walitoka miradi ya maarifa huria kama vile KIWIX na miradi ndani ya Wikimedia kama vile Wiki Loves Africa, Wiki Loves Women, WikiFundi (programu za kuhariri Wikipedia bila intaneti).

Ratiba[hariri | hariri chanzo]

Ratiba ya mkutano ilikazia ushirikiano kati ya taasisi mbalimbali zinazokazia maarifa huria kama vile Wikimedia (pamoja na Wikipedia na Wikimedia Commons), Kiwix na nyingine.

Suala lingine lililokaziwa ni namna ya kupata wahariri wapya. Wanamkutano walisikia taarifa ya utafiti kuwa jina la Wikipedia halijulikani katika nchi mbalimbali za Asia na Afrika. Katika nchi kama Nigeria na India watu wengi, na hata watumiaji wengi wa intaneti, bado hawajajua jina la Wikipedia.

Taarifa nyingine zilionyesha jinsi gani milango iko wazi kwa ushirikiano kati ya Wikipedia na taasisi kama makumbusho, vyuo na shule katika nchi kama vile Afrika Kusini, Cote d'Ivoire, Tunisia au Misri. Katika nchi hizo kuna vikundi vya watumiaji wanaokutana na kushirikiana.

Hali ya Wikipedia katika Afrika ya Mashariki[hariri | hariri chanzo]

Washiriki kutoka nchi hizi walikuwa wachache mno. Mwakilishi wa Wikipedia ya Kiswahili alikuwa Mtumiaji:Kipala anayeishi Ujerumani. Kutoka Dar es Salaam alikuja Mtumiaji:Bukulu_Steven aliyewahi kushiriki katika miradi ya Wikimedia huko Uganda. Kutoka Kenya hapakuwa na mwanawikipedia lakini alikuwapo mwakilishi wa mradi wa Creative Commons anayeshughulikia mambo ya leseni za maarifa huria kwa Afrika pamoja na miradi kama Wikipedia zero. Habari nzuri ilikuwa ya kwamba kundi la watumiaji wa Wikipedia limeanzishwa Dar es Salaam siku chache kabla ya WikiIndaba kutokana na ziara ya afisa wa Wikimedia huko.

Kwa sasa watumiaji kutoka Tanzania waliochangia mengi katika Wikipedia ni wahariri 2 wa Wikipedia ya Kiswahili wanaoishi Dar na Morogoro. Huko Kenya mtumiaji aliyechangia mengi katika Wikipedia ya Kiswahili ni mtumiaji:ChriKo.

Habari moja ya kutia moyo ilipatikana katika somo juu ya Wikipedia kwa lugha za Kiafrika ambapo imeonekana ya kwamba watumiaji wa Wikipedia nchini Tanzania wanachagua mara nyingi kurasa za sw.wiki kulingana na kuangalia en.wiki kama makala ziko kuhusu mahali ndani ya nchi (hata kama en.wiki bado inatazamwa zaidi).

Mkutano ujao[hariri | hariri chanzo]

Mkutano ujao mnamo mwaka 2019 utafanyika Tunisia. Kuna tumaini la kwamba hadi wakati ule jumuiya ya wanawikipedia itakua na wajumbe zaidi kutoka Afrika ya Mashariki wataweza kutumwa.

Tazama Pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]