WikiFundi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mwongozo kwa watumiaji (toleo la vanilla)

WikiFundi ni programu ambayo inatoa mazingira ya kuhariri Wikipedia bila kutumia mtandao wa intaneti. WikiFundi inaruhusu watu kuchangia kuandika makala za Wikipedia hata wakati hakuna mtandao au umeme. Inawezesha watu, makundi na jumuiya kujifunza jinsi ya kuhariri Wikipedia na kufanya kazi kwa kushirikiana. Mara baada ya kukamilika kwa makala na kuwa na mtandao wa intaneti, makala hizi zinaweza kupakiwa kwenye Wikipedia.

Programu hiyo iliundwa kusaidia vuguvugu la WikiAfrica na wahariri wa kujitolea wa Wikimedia barani Afrika. Walioiunda ni Florence Devouard na Isla Haddow-Flood. Programu inatekelezwa na Emmanuel Engelhart (Kelson), Anthere na wanachama wengine wa jamii. Maendeleo ya programu yanasaidiwa na Taasisi ya Orange. Programu ya WikiFundi na nyaraka zake ziko chini ya leseni CC-BY-SA 4.0.

Viungo vya kupakua programu[hariri | hariri chanzo]

Tech ReadMe

Mwongozo wa watumiaji

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]