Seleuko I

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Seleuko I
binadamu
Jinsiamume Hariri
Nchi ya uraiaMacedonia, Seleucid Empire Hariri
Jina halisiΣέλευκος Hariri
Cheo cha heshimaMfalme, Basileus Hariri
Tarehe ya Kuzaliwa358 BCE Hariri
Mahali alipozaliwaEuropos Hariri
Tarehe ya kifo281 BCE Hariri
Mahali alipofarikiLysimachia Hariri
Chanzo cha kifoUuaji Hariri
Aliuawa naPtolemy Ceraunus Hariri
Sehemu ya kuzikwaSeleukia Hariri
BabaAntiochus Hariri
MamaLaodice of Macedonia Hariri
NduguDidymeia Hariri
MwenziApama, Stratonice of Syria Hariri
MtotoAntiochus I Soter, Phila, Achaeus Hariri
FamiliaSeleucid dynasty, Seleucid Empire Hariri
Lugha zinazozungumzwa, zilizoandikwa au zilizotiwa sahihiKiyunani Hariri
Kazisovereign Hariri
Nafasi ilioshikiliwaSeleucid ruler Hariri
DiniAncient Greek religion Hariri
Depicted byAntigonos Monop"hthalmos statue at Olympia" Hariri
Sanamu ya Seleuko I.
Maeneo yaliyotawaliwa na Seleuko I.

Seleuko I Mshindi (kwa Kigiriki: Σέλευκος Νικάτωρ Seleukos Nikator yaani "mshindi"; mnamo 358 KK hadi 281 KK) alikuwa afisa Mgiriki kutoka Makedonia ambaye alikuwa kati ya waandamizi wa Aleksander Mashuhuri.

Seleuko alianzisha Milki ya Waseleuko iliyoendela kutawala sehemu kubwa ya Mashariki ya Kati kwa karne zilizofuata hadi ilipotekwa na Dola la Roma mnamo mwaka 63 KK.

Katika jeshi la Aleksander, Seleuko alikuwa mkuu wa kikosi muhimu akaongozana na jeshi hadi Uhindi. Kwenye siku zake za mwisho, Aleksander Mashuhuri aliamuru kuwaoza wanajeshi wake na wanawake wa Kiajemi kwa shabaha ya kuunda umoja katika milki yake kubwa. Seleuko alipewa binti kutoka sehemu za Afghanistan; ndoa hiyo ilikuwa ndoa pekee iliyodumu kati ya majenerali wote wa Aleksander waliolazimishwa wakati ule kumkubali mke mpya. Bila shaka ilimsaidia baadaye kutawala Uajemi.

Katika mapambano baada ya kifo cha Aleksander, Seleuko alitoka kama mtawala wa Asia Ndogo, Syria, Mesopotamia na nyanda za juu za Uajemi hadi kutumia rasmi cheo cha basileos yaani mfalme. Milki aliyoianzisha iliendelea kuwa moja ya madola makuu katika enzi ya Uheleni hadi kushindwa hatimaye na Dola la Roma na uenezi wa Milki ya Parthia.

Baada ya kifo cha Aleksander mnamo Juni 323 KK, Seleuko alimwunga mkono Perdika aliyekuwa mtawala naibu baada ya Aleksander. Aliteuliwa naye kuwa naibu mkuu wa Babeli. Katika mwaka uliofuata baada ya kifo cha mfalme, vita ya waandamizi ilianza na Seleuko alimfuata Perdika katika uvamizi wa Misri dhidi ya Ptolemaio I. Wakati askari wa jeshi walianza kugoma, Seleuko alishiriki katika kumwua Perdika. Kwenye mkutano wa majenerali wa Aleksander uliofuata mwaka 320 KK, Seleuko alipewa nafasi ya gavana kamili wa Babeli.

Lakini vita baina ya waandamizi wa Aleksander Mashuhuri ziliendela na hapo Seleuko alipaswa kukimbia na kujificha. Alipoweza kurudi Babeli mnamo mwaka 312 KK alishika tena mamlaka juu ya Mesopotamia akaeneza mamlaka yake hadi nyanda za juu za Uajemi na hadi Syria. Kwa hiyo alitawala hatimaye sehemu yote ya mashariki ya milki ya Aleksander.

Upande wa mashariki, Seleuko alijaribu kudhibiti pia maeneo yaliyotekwa na Aleksander huko Bara Hindi. Lakini alikuta Milki ya Maurya iliyowahi tayari kuvamia majimbo hayo. Hatimaye Seleuko alipatana na mfalme wa Kihindi Chnadragupta Maurya, akamwachia majimbo hayo na kumpa binti yake kama mke[1]. Maurya alimshukuru kwa kumpatia Seleuko kikosi maalumu wa tembo wa vita 500 pamoja na viongozi wao kilichomsaidia kushinda maadui yake katika magharibi na kuongeza Asia Ndogo katika himaya yake.

Mwishoni Seleuko aliuawa wakati wa vita katika Ugiriki; mwuaji wake alikuwa mwana wa mfalme wa Misri Ptolemaio I aliyewahi kukimbia Misri. Mwuaji huyu Ptolemaio Keranos aliendelea kutawala Makedonia yenyewe.

Seleuko alifuatwa katika ufalme na mwanawe Antioko I kuwa mtawala wa Milki ya Waseleuko.

Sarafu ya Tetradrakmu, inamwonyesha Seleuko I, mwenye pembe za fahali. Nyuma: Mungu wa Kiroma Apollo, akiwa na upinde, ameketi.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Appian, p. 55.

Marejeo na kusoma zaidi[hariri | hariri chanzo]