Nenda kwa yaliyomo

Nyanda za Juu za Iran

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya picha za hali ya juu za Irani zilizo na mipaka ya kisasa.

Nyanda za Juu za Iran, pia za Uajemi (kwa Kiajemi: فلات ایران) [1] [2] ni eneo la milima katika Asia ya Magharibi, kati ya Mesopotamia upande wa magharibi na milima ya Hindu Kush upande wa mashariki.

Mipaka na jina[hariri | hariri chanzo]

Mpaka wa kaskazini wa nyanda za juu upo Asia ya Kati. Upande wa kusini mipaka iko Ghuba ya Uajemi, mlangobahari wa Hormuz na Ghuba ya Oman.

Nyanda hizo za Juu zinaenea ndani wa Iran, pamoja na sehemu za Afghanistan, Azerbaijan, Pakistan, Turkmenistan na Iraq[3].

Ramani ya kijiografia

Mazingira na jiolojia[hariri | hariri chanzo]

Panda mipaka katika eneo la Asia ya Kati

Nyanda za Juu zilitokana na bamba la gandunia la Iran ambalo ni sehemu ya bamba la Ulaya-Asia, inayobanwa kati ya mabamba ya Uarabuni na ya Uhindi.

Iko ndani ya ukanda wa milima inayoenea kutoka Hispania hadi Himalaya, ukipitia nyanda za juu za Anatolia, milima ya Kaukazi na kuendelea katika milima ya Hindu Kush, Pamir na Himalaya.

Nyanda za juu za Iran zinavirigishwa na milima kunjamano ambayo ni Milima ya Alborz upande wa kaskazini, Kopet Dag na Aladağlar upande wa mashariki, halafu Milima ya Zagros upande wa magharibi na kusini-magharibi. Upande wa kusini-mashariki, nyanda za juu huishia kwenye milima ya Kuh-e Jebal Barez, Kuh-e Birag, Kuh-e Taftan na Kuh-i Sultan ya Baluchistan.

Kutokana na miendo ya gandunia eneo lote la nyanda za juu za Iran linaathiriwa mara kwa mara na mitetemeko ya ardhi.

Nyanda za juu zinagawanywa na safu za pembeni za Zagros zinazoelekea kutoka kaskazini-magharibi kwenda kusini-mashariki: Kuh-e Rud, Kuh-e Davaran na Kuh-e Banan.

Kati ya safu ya milima na mto Kuhrud kuna majangwa makubwa ya Iran ambazo ni Dasht-e Lut, Dasht-e Kawir, Rigestan, Dasht-e Margoh, Jaz Mirian na Hamum-i Mashkel.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. The archaeological evidence of the second millennium B.C. on the Persian plateau. ISBN 0-521-07098-8.
  2. A System of Geography, Popular and Scientific (1832), Archibald Fullarton, pp 7, 284, 287, 288
  3. Artikel Iranian highlands, in: Britannica.
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nyanda za Juu za Iran kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.