Omukama

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Omukama ni cheo alichopewa kiongozi mkuu wa kabila la Wahaya (na Wanyambo) mkoani Kagera nchini Tanzania. Mfano wake ni Kabaka wa Waganda.

Neno hili kwa Kihaya na Kinyambo lina maana ya mkuu au mfalme, na jina la kiongozi huyo aliitwa Lumanyika.

Koo-Mtwale, mkuu wa himaya au sehemu iliyo chini ya Mkama. Mtwale anamwakilisha Omkama kwa shughuli za kimila na sheria. Mtwale mara nyingi anaamua kesi ndogondogo kama za ndani ya ndoa, koo, wizi na ugomvi wa majirani na watu.

Lakini kuna sehemu kama za eneo la Kiziba ambalo lilikuwa na mfalme wake ambaye alichagua viongozi wa hadhi ya juu, ambao waliitwa Omulangila kwa mwanamume na Omwana kwa mwanamke, ambao waliongoza sehemu kubwa la eneo la Mkama na mara nyingi walikuwa wenye mali, fedha na mashamba makubwa ambao watu walienda kuomba kazi mbalimbali kwao kama vibarua na kulima na kuchunga ng’ombe.

Kwa sehemu za Kihanja na Ihangilo wafalme wao walikuwa kama hao na walikuwa mara nyingi wenye uwezo mkubwa na koo maarufu.

Elimu: kuingia kwa wamisionari katika karne ya 19 ambao walianzisha shule nyingi za awali na za kati ambapo ilibidi mtu abatizwe ili aweze kupata elimu. Wazazi wengi walipeleka watoto wao kubatizwa na hapo kukaanza mvutano, sababu wamisionari walikuwa Wakatoliki kutoka Ufaransa na Uswisi na Walutheri kutoka Ujerumani na Uholanzi. Ndipo kukaanza mashindano ya kuanzisha shule nyingi ili kupata waumini wengi.

Wamisionari pia wakawa mstari wa mbele kufungua hospitali nyingi kila wilaya na vyuo vya ufundi.

Ndiyo maana maeneo hayo ya Kagera elimu ni ya juu kwa wakazi wake na huduma za afya kuliko mikoa jirani. Na kilimo cha kahawa kiliwapa wenyeji fedha za kujenga nyumba bora na kupeleka watoto wao kwenye elimu ya juu zaidi. Pia kulianzishwa chama cha ushirika cha mkoa ambacho kilianzisha shule za watoto wa wakulima kuwasomesha na kutoa mikopo. Eneo hilo lilizidi kurutubishwa kushinda maeneo mengine mengi ya nchi kutoa Uchagga.

Pia wamisionari walianzisha seminari na chuo cha kutoa mapadri wao wenyewe.

Waarabu walioleta Uislamu walikuwa wanakazania sana biashara, si shughuli za maendeleo ya watu.

Blank template.svg Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Omukama kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.