Kabaka

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Muwenda Mutebi II ni Kabaka wa Buganda tangu mwaka 1993
Sylvia Nagginda ambaye ni malkia (Nnabagereka) wa Buganda akivaa mapambo ya Kisamburu wakati wa kutembelea Kenya mnamo mwaka 2003

Kabaka ni cheo cha mfalme wa Buganda ambayo ni ufalme ndani ya jamhuri ya Uganda. Cheo kingine pamoja na Kabaka ni Ssebataka.

Tangu mwisho wa karne ya 19 Makabaka wamekuwa Wakristo Waanglikana wakipokea taji katika kanisa kuu la Kianglikana la Kampala. Makabaka wa mwisho wamezikwa katika makaburi ya Kasubi mjini Kampala.

Serikali ya kwanza ya Milton Obote ilifuta falme zote nne za Uganda na kumlazimisha Kabaka Mutesa II kuondoka Uganda akipata kimbilio lake Uingereza.

Kati ya 1967 hadi 1993 cheo cha Kabaka hakikuwepo kisheria nchini Uganda lakini Waganda wengine walisikitikia. Serikali ya Yoweri Museveni ilirudisha falme za kale kama enzi za kiutamaduni.

Tarehe 24 Julai 1993 Ronald Muwenda Mutebi II aliruhusiwa kurudi Uganda kutoka Uingereza alikokuwa amemfuata baba yake akapokea rasmi taji la Kabaka mjini Kampala.

Makabaka wa Buganda[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]