Samburu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Samburu
Maeneo yenye Idadi ya Watu yenye Maana
north central Kenya
Samburu pia yaweza kumaansha lugha ya Samburu, Hifadhi ya kitaifa Samburu au Wilaya ya Samburu

Samburu au Kisamburu ni kabila ya kundi la Nilote ambao kwa sasa wanapatikana kati ya kaskazini ya Kenya na ambao wanauhusiana lakini ni tofauti na Wamaasai. Wasamburu ni wafugaji ambao ni wanomadi ambao hufuga mifugo hasa ng'ombe, lakini pia hufuga kondoo, mbuzi na ngamia. Jina ambalo wanaitumia wao wenyewe ni Lokop au Loikop , jina ambalo linaweza kuwa na maana mbalimbali ambayo Wasamburu wenyewe hawawezi kukubaliana. Wengi wanadai kwamba jina hili linamaanisha "wamiliki wa nchi" ( "lo" inamaanisha umiliki, "nkop" ni nchi au ardhi), ingawa wengine wanatoa tafsiri tofauti sana ya jina hilo. Wasamburu huzungumza lugha ya Kisamburu ambayo ni lugha ya Nilo-Sahara. Kuna pia Hifadhi ya wanyama katika eneo hilo, Hifadhi ya wanyama ya Samburu.

Makao yao[hariri | hariri chanzo]

Wanaishi kaskazini ya ikweta katika wilaya ya Samburu, eneo ambalo ni eneo a eneo maili 8000 (eneo a eneo kilomita 21.000). Ardhi yao ni ya utofauti kuu na ni rembo. Kabla na miaka michache baada ya uhuru eneo hili lililoko kaskazini mwa ikweta lilikuwa linajulikana kama Northern Frontier District (NFD). Wilaya ya Samburu wakati moja ilikuwa sehemu kubwa ya NFD. Ni Viongozi wa serikali tu ambao waliruhusiwa kuingia na ilikuwa imefungiwa wageni wote wenye ukoo wa Kiulaya na ukoo wa Kiafrika. Kibali maalum kilichotolewa na utawala kilihitajika kuonyeshwa ili kuingia katika sehemu ya NFD. Hata leo sehemu ya Samburu bado ni eneo la mashambani.

Utamaduni[hariri | hariri chanzo]

Mashujaa wa Wasamburu karibu na Ziwa Turkana.

Jina[hariri | hariri chanzo]

Wasamburu ni sehemu ya watu wanaozungumza lugha ya Maa. Wamasai pia ni watu wa Maa. Karibu 95% ya maneno ya lugha zote mbili ni sawa. Jina la 'Samburu' ni pia ni asili ya Kimasai na imechukuliwa kutoka neno 'Samburr' ambayo ni mfuko wa ngozi unaotumiwa na Wasamburu kubeba vitu mbalimbali. Haieleweki ni wakati gani Kisamburu ikawa kabila inayotambulika rasmi. Kama jambo la kawaida katika sehemu nyingi duniani kote, Kabila zinazotambulika zikawa fasta na kufafanuliwa wakati walikumbana wa Wakoloni. Wasafiri kutoka Ulaya katika karne ya 19 mara nyingi walikuwa wanawaita Wasamburu "Burkineji" (watu wa mbuzi weupe), na kuna uhusiano nyingi na makabila jirani. Baadhi ya Wasamburu wanaukoo kutoka kwa Wamaasai Laikipiak waliobaki, sehemu ya Wamaasai iliyoharibiwa mwishoni mwa karne ya 19. Wengine wanatoka katika makabila ya Kirendille, Kiturkana na Kiborana.

Uchumi[hariri | hariri chanzo]

Kimila uchumi wa Wasamburu ulikuwa ufugaji, huku wakijitahidi kuishi kwa bidhaa ya mifugo yao ya ng'ombe, mbuzi na baadhi ya ngamia. Hata hivyo, muungano wa ukuaji adhimu wa idadi ya watu katika kipindi cha miaka 60 na kushuka kwa idadi ya wanyama wanaowamiliki imewalazimu kutafuta njia zingine tofauti za kuishi. Baadhi yao wamejaribu kupanda mazao, huku wanaume wengi ambao ni vijana wamehama angalau kwa vipindi vifupi kwa miji kuu ilikufanya kazi na kupata mapato. Wengi wanafanya kazi katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, kama Walinzi, huku pia ni maarufu kupata wengine wao katika mahoteli ya pwani ya Kenya ambapo baadhi yao kazi; wengine wao huuza mikuki na mapambo.

Nyumba[hariri | hariri chanzo]

Wasamburu hushiriki katika ndoa ya wake zaidi ya moja, na mwanaume anaweza kuwa na wake zaidi ya moja. Makazi ya Kisamburu inajulikana kama nkang (Maa) au manyatta (Kiswahili). Inaweza kujumuisha familia moja tu, lililoundwa na mwanaume na mkewe / wakewe. Kila mwanamke ana nyumba yake binafsi, ambayo huijenga kwa msaada kutoka kwa wanawake wengine kutoka kwa nyenzo za mitaa, kama vile vijiti, matope na kinyesi cha ng'ombe. Makazi Kubwa ya ibada, yanayojulikana kama lorora huweza kujumuisha familia 20 au zaidi. Hata hivyo, makazi hujumuisha sanasana familia mbili au tatu, pamoja na labda nyumba 5-6 ambao hujengwa katika mviringo huku nafasi wazi ikiachwa katikati mwa mviringo huo Mzunguko wa manyumba imezungukwa na ua la miiba na katikati mwa kijiji kuna pahala pa wanyama mbali na wanyama wanaokula wenzao.

Mavazi[hariri | hariri chanzo]

Wanaume huvalia nguo ambayo mara nyingi nyekundu au samawati na nguo hufungwa kwa kuizungusha kiunoni. Wao pia hujipamba kwa shanga na vikuku, kama Wamaasai. Nywele zao, ambazo ni ndefu, mara nyingi ni nyekundu na kusukwa kwa makini katika vichwa vyao Miili yao mara nyingi hupakwa rangi ya ochre. Wanawake kuvalia vipande viwili vya kitambaa vya rangi ya samawati au zambarau, , kipande kimoja kikiwa kimefungwa kiunoni, na kipande cha pili kikiwa kimefungwa kifuani. Wanawake huwa na upara na kuvalia shanga mbalimbali na vikuku. Chakula

Chakula[hariri | hariri chanzo]

Kimila Wasamburu walitegemea sana mifugo yao. Chakula kuu cha kimila kilikuwa maziwa, ambacho kwa siku ya kawaida kingejumuisha kwa ukamilifu mlo wao. Maziwa ya ng'ombe huhafadhlishwa. Kondoo na mbuzi pia hukamuliwa, ingawa wengi hufikiria kuwa maziwa yao ni dhaifu au hufaa zaidi kwa matumizi ya chai. Katika maeneo ya ukame ambapo ngamia ni maarufu maziwa yao hupendwa sana, lakini Wasamburu ambao hawafugi ngamia husema kuwa maziwa hii si nzuri kwa matumizi kama chakula. Maziwa inaweza kunywewa aidha kama ni “fresh” au “fermented” na maziwa " iliyoiva " mara nyingi kufikiriwa kuwa kuu. Nyama kutoka kwa ng’ombe huliwa sanasana katika hafla za sherehe au wakati ng'ombe huaga dunia. Nyama kutoka wanyama ndogo ni huliwa zaidi kwa kawaida, ingawa bado si mara kwa mara. Leo, Wasamburu hutegemea sana bidhaa za kilimo zilizonunuliwa - pamoja na pesa wanazopata kutokana na mifugo yao wanayouza - na hasa unga wa mahindi ambayo hutumika kutengeneza uji. Chai pia ni mlo wa kawaida na hunywewa kwa kiasi kikubwa cha sukari na (ikiwezekana) maziwa, na kwa kweli ni mlo mkuu wa kisasa wa Wasamburu. Damu ni huchukuliwa kutoka kwa wanyama waliohai na pia hukusanywa kutoka kwa wale wanyama waliochinjwa. Kuna njia angalau 13 za kuandaa au kutayarisha damu na la ajabu ni kwamba damu inaweza kuunda mlo mzima! Baadhi ya Wasamburu [1] siku hizi wamegeuka na kuanza kushiriki katika kilimo, pamoja na matokeo tofauti.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Jon Holtzman, Uncertain Tastes: Memory, Ambivalence and the Politics of Eating in Samburu, Northern Kenya. (2009, University of California Press).