Mwanakondoo wa Mungu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mwanakondoo akishika bendera ya Kikristo ni ishara ya'Yesu.
Agnus Dei ya Karne za kati katika Basilika la Parenzo, Korasia.

Mwanakondoo wa Mungu ni neno la Injili ya Yohane (1:29, 36) lililotamkwa na Yohane Mbatizaji kumhusu Yesu Kristo ili kumtambulisha kama kafara itakayotolewa kwa ukombozi wa binadamu wote: kwamba atabeba dhambi ya ulimwengu na kuifidia kwa kujitoa kabisa.

Kwa Kilatini neno hilo ni Agnus Dei na linatumika kutajia mchoro wa mwanakondoo mwenye msalaba (au bendera ya msalaba) ukiwa ishara ya Kristo.

Agnus Dei ni pia jina la litania fupi ambayo inaanzia na maneno hayo na kutumika wakati wa Misa padri anapomega hostie takatifu na kuchanganya kipande na umbo la divai lililomo katika kikombe.