Robert Mugabe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mugabe)
Jump to navigation Jump to search
Robert Mugabe (2009)

Robert Gabriel Mugabe (* 21 Februari 1924) amekuwa kiongozi wa Zimbabwe tangu 1980. Yeye ni mwenyekiti wa chama tawala cha ZANU. 1980 alikuwa waziri mkuu na 1987 Rais wa Zimbabwe. Kabla ya wakati ule aliongoza upinzani wa ZANU dhidi ya serikali ya walowezi Waingereza nchini waliofuata siasa ya ubaguzi wa rangi.

Mugabe alirudiwa katika uchaguzi mbalimbali. Tangu mwaka 2000 uchaguzi hizi zimekuwa mashakani kutokana na matishio na matumizi ya mabavu dhidi ya wapinzani. Utawala wa Mugabe umeitwa wa kidikteta tangu mwaka 2002. Kutokana na mashataka dhidi ya serikali ya Mugabe ya kudharau haki za binadamu nchi Zimbabwe ilisimamishwa ndani ya Jumuiya ya Madola. Mugabe pamoja na mawaziri wake na viongozi wa chama chake hawaruhusiwi kusafiri kwenda nchi za Umoja wa Ulaya na Marekani.

Mwanzoni wa utawala wake Mugabe alisifiwa kujenga uchumi na sera ya elimu nchini. Zimbabwe ilikuwa nchi iliyouza vyakula vingi nje. Tangu mwanzo wa milenia mpya pamoja na mashtaki ya udikteta hali ya uchumi ulirudi nyuma. Takriban milioni mbili za raia wa Zimbabwe wameondoka nchini wakikaa kama wakimbizi Afrika Kusini.


Tuhuma za mauaji na ukandamizaji

Baada tu ya kushika madaraka, Mugabe aliamua kuimarisha jeshi lake la kumlinda (liitwalo Gukurahundi) ambalo lilijengwa na watu kutoka kabila lake la wa-Shona. Nchi hiyo ilikuwa tayari imegawanyika kikabila hata katika uchaguzi wa kwanza wa 1980, washona wote walimchagua Mugabe na Wa-Ndebele na wabunge kutoka chama cha ZANU. Wakati wandebele walichagua viongozi kutoka chama cha ZAPU kilichoongozwa na Joshua Nkomo.

Mara baada ya uchaguzi tu mwezi Novemba 1980 Mugabe alianza kampeni ya kuua kwa wingi watu wa kabila la wa-Ndebele ambao mjia wao mkubwa unaitwa Bulawayo. Ingawa mauaji hayo hayakufikia kiwango cha yale ya Rwanda na Burundi, waliuawa wanawake, wanaume, watoto na hata vichanga vilivyokuwa matumboni. Mwaka 1981 pia Mugabe aliendelea kuua wandebele tukio ambalo halikutangazwa sana na vyombo vya habari. Kuanzia enzi hizo hadi leo raisi Mugabe amejaribu kushinda kila uchaguzi unaokuja nchini huko kwa kutumia nguvu za kikabila na mabavu.

Mugabe ametangazwa upya na chama cha ZANU kama mgombea wa urais katika uchaguzi wa 2008.

Administradors.png Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Robert Mugabe kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.