Gukurahundi
Gukurahundi ni neno la lugha ya Kishona linalozungumzwa nchini Zimbabwe linalomaanisha "kufyeka, kusafisha".
Neno hilo lilitumiwa pia kisasa katika historia ya chama cha ZANU kwa kumaanisha takaso la kisiasa ambako kada wa chama waliotazamwa hawakubali na uongozi waliondolewa madarakani na wakati mwingine kuuawa.
Gukurahundi wa 1982-1984
[hariri | hariri chanzo]Baada ya uhuru wa Zimbabwe mwaka 1980 kulikuwa na hali ya kutoelewana baina ya wafuasi wa vyama vilivyowahi kupigania uhuru, ZANU na ZAPU. Vyote viwili vilikuwa na asili moja, ila vilifarakana kuhusu mbinu za kupambana na utawala wa kikoloni. Tofauti za kisiasa ziliongezewa ukali na tofauti za kabila maana kada wengi wa ZANU walikuwa Washona ilhali ZAPU chini ya Joshua Nkomo ilikuwa hasa na Wandebele.
Waziri mkuu Robert Mugabe wa ZANU alihofia upinzani upande wa ZAPU, hivyo aliandaa kikosi cha pekee katika jeshi jipya la Zimbabwe lililokuwa maarufu kama Brigedi ya Tano lililofundishwa na walimu wa kijeshi kutoka Korea Kaskazini. Mugabu alituma brigedi hiyo mwaka 1982 katika nchi ya Wandebele ili watafute kada za ZAPU na jeshi lake ZIPRA. Katika kampeni hiyo watu 20,000 waliuawa hovyo. Nkomo alikimbilia Uingereza.
Baada ya mapatano ya amani na maungano ya vyama vya ZANU na ZAPU kwenye mwaka 1987 mauaji ya Gukurahundi yalichunguliwa lakini matokeo ya utafiti yalifichwa.
Baada ya kupinduliwa kwa Mugabe mwaka 2019 rais mpya Emmerson Mnangagwa alitangaza majadiliano ya kitaifa kuhusu kipindi cha Gukurahindi[1]. Makaburi ya makundi ya wakati ule yamefunguliwa na maiti kuzikwa upya [2].
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Gukurahundi: Can the man accused of opening the wounds heal them?, tovuti ya africanarguments, iliangaliwa 11-09-2019
- ↑ Zimbabwe begins exhuming victims of Gukurahundi massacre, gazeti la Mail and Guardian, Afrika Kusini, 30 Apr 2019
Kujisomea
[hariri | hariri chanzo]- Mukiwa: A White Boy in Africa, Part Three, Peter Godwin, Picador, ISBN 0-330-45010-7
Filamu
[hariri | hariri chanzo]- Documentary Film: Finding Mercy (director: Robyn Paterson, 2012) includes interviews with Zimbabwean civilians and refugees about Gukurahundi and the policy of Mugabe
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- "Breaking the Silence, Building True Peace. A report on the disturbances in Matabeleland and the Midlands 1980–1989"
- Independence: Twenty years on Archived 7 Desemba 2006 at the Wayback Machine. Cry Zimbabwe tells how Robert Mugabe and his ZANU-PF came to political power after British and Commonwealth supervised elections in 1980.
- Fifth Brigade Gukurahundi atrocities Youtube
- Ian Smith's Comments during Gukurahundi Youtube
- Matabeleland Testimonies – 1983 Youtube
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Gukurahundi kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |